Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yesu Aliwekwa Lini Kuwa Mfalme?
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 1
    • 2. Ufalme wa Mungu ulikosa kuwakilishwa duniani kwa muda gani?

      Muda mfupi baada ya Yerusalemu kuharibiwa, Yehova alimwambia nabii wake Danieli kwamba Mungu angemchagua mfalme ambaye angetawala kutoka mbinguni. Utawala huo ungeanza lini?​—Soma Danieli 7:13, 14.

      Danieli alifasiri maono ambayo Mungu aliagiza kwamba mti mkubwa ukatwe, kama vile tu Mungu alivyokuwa ameamuru ufalme uliokuwa Yerusalemu ukatwe na kuharibiwa. Lakini mizizi ya mti huo haingeng’olewa ili baada ya “nyakati saba” mti huo ukue tena. Biblia inaonyesha kwamba “nyakati” tatu na nusu ni sawa na siku 1,260, hivyo “nyakati saba” ni sawa na siku 2,520. (Ufunuo 12:6, 14) Katika unabii wa Biblia, mara nyingi siku huwakilisha miaka. (Hesabu 14:34) Hivyo, Ufalme wa Mungu haungekuwepo duniani kwa miaka 2,520.​—Soma Danieli 4:10-17.

      3. Yesu alianza lini kutawala akiwa Mfalme?

      Mungu alimtawaza Yesu kuwa Mfalme mbinguni mwaka wa 1914, miaka 2,520 kamili baada ya Yerusalemu kuharibiwa. Hatua ya kwanza ambayo Yesu alichukua akiwa Mfalme ni kumfukuza Shetani na roho wake waovu kutoka mbinguni. (Ufunuo 12:7-10) Tukio hilo halikuonekana kwa macho ya wanadamu, lakini matokeo yake yalikuwa msukosuko ambao ulionekana. (Ufunuo 12:12) Mambo ambayo yamekuwa yakitukia tangu 1914 yanathibitisha kwamba huo ndio mwaka ambao Yesu alitawazwa kuwa Mfalme.​—Soma Mathayo 24:14; Luka 21:10, 11, 31.

  • Yesu Aliwekwa Lini Kuwa Mfalme?
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 1
    • [Chati katika ukurasa wa 16, 17]

      (Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

      Oktoba Oktoba

      607 K.W.K.. 1914 W.K.

      ← Miaka 2,520 →

      1000 K.W.K. 1 K.W.K. 1 W.K. 1000 W.K. 2000 W.K.

      ← Miaka 606.25 →← Miaka 1,913.75 →

      Kuharibiwa kwa Tumia kifaa cha Mungu amfanya Yesu

      ufalme uliokuwa kufanya hesabu: kuwa Mfalme mwenye

      Yerusalemu 606.25 mamlaka juu

      + 1,913.75 ya mataifa

      = 2,520

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki