Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Hivyo, mnamo 1928, ofisi ya tawi ilinunua mashua yenye injini, ambayo ingewatosha mapainia wawili au watatu na yenye nguvu inayoweza kuabiri pwani ya Norway iliyochongoka sana. Lakini nani angekuwa nahodha wa mashua hiyo? Karl Gunberg, painia mwenye uzoefu alijitolea. Ujuzi wake alipokuwa katika jeshi la wanamaji na pia akiwa mwalimu wa mambo ya usafiri ulimsaidia sana. Mashua ya kwanza iliyoitwa Elihu, ilianza safari huko Oslo, ikaelekea kaskazini huku ikitia nanga katika bandari mbalimbali. Hata hivyo, usiku mmoja wa majira ya baridi kali ya mwaka wa 1929, kulitokea dhoruba kubwa iliyoiharibu mashua hiyo karibu na Stavanger. Wote walishukuru kwamba ndugu katika mashua hiyo walifika ufuoni salama.

      Mnamo 1931 ndugu walipata mashua nyingine waliyoiita Ester. Kwa mara nyingine tena, Karl akashika usukani akisaidiwa na ndugu wengine wawili. Ester ilitumiwa magharibi na kaskazini mwa Norway kwa miaka saba iliyofuata. Mwaka wa1932, Karl alihisi kwamba “amezeeka na hivyo hawezi kuendelea na safari hizo.” Kwa hiyo, akamwachia Johannes Kårstad usukani na akatumika akiwa painia katika eneo la mashariki mwa Norway.

  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 114]

      Karl Gunberg alikuwa nahodha wa mashua iliyoitwa “Elihu”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki