-
Je, Hilo Pigano Linafanikiwa?Amkeni!—1996 | Januari 8
-
-
Takataka yenye kutisha kuliko zote ni taka za unururishi, matokezo ya vituo vya nguvu za nyukilia. Maelfu ya tani za taka za nyukilia zimewekwa katika mahali pa muda, ingawa nyingine tayari zimetupwa katika bahari-kuu. Ijapokuwa miaka mingi ya utafiti wa kisayansi, bado suluhisho halijapatikana la kuhifadhi kwa njia salama yenye kudumu, na hakuna lolote litapatikana karibuni. Hakuna ajuaye ni lini unururishi huenda ukatokeza madhara. Hatari hii ya kimazingira kwa hakika haitatoweka—hizo taka zitakuwa zenye unururishi kwa karne nyingi ama mileani zijazo, au mpaka Mungu atakapochukua hatua.
-
-
Je, Hilo Pigano Linafanikiwa?Amkeni!—1996 | Januari 8
-
-
Tatizo lenye kuogopesha la kukosa mahali pa kutupa taka za nyukilia ni kikumbusha cha kwamba sayansi si yenye uwezo wote. Kwa miaka 40 wanasayansi wamekuwa wakitafuta maeneo salama ya kudumu ya kuhifadhia taka zenye unururishi mwingi. Huo utafutaji unathibitika kuwa mgumu sana hivi kwamba nchi nyingine, kama vile Italia na Argentina, zimefikia mkataa kwamba hazitapata mahali kama hapo hadi kufikia mwaka wa 2040 ikiwa ni mapema mno. Ujerumani, nchi iliyo na mtazamo chanya zaidi katika nyanja hii, yatumaini kukamilisha mipango kufikia mwaka 2008.
Kwa nini taka za nyukilia ni tatizo hivyo? “Hakuna mwanasayansi ama mhandisi awezaye kutoa uhakikisho kamili kwamba taka zenye unururishi hazitavuja siku fulani kwa viwango hatari hata kutoka kwenye mabohari yaliyo bora zaidi,” aeleza mwanajiolojia Konrad Krauskopf. Lakini licha ya maonyo ya mapema kuhusu hilo tatizo la kutupa taka, serikali na viwanda vya nyukilia mbalimbali zilipiga hatua mbele bila uangalifu, zikidhania kwamba tekinolojia ya usoni ingetokeza suluhisho. Wakati huo wa usoni haukufika kamwe.
-