Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mafuta Hutoka Wapi?
    Amkeni!—2003 | Novemba 8
    • Kadiri miaka inavyopita, biashara ya mafuta imesitawi sana ulimwenguni kwa sababu ya kugunduliwa kwa maeneo mapya ya mafuta katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Maeneo 50,000 hivi yamepatikana! Hata hivyo, kiasi cha mafuta hakitegemei idadi ya maeneo lakini kinategemea ukubwa wa maeneo hayo. Ni makubwa kadiri gani?

      Maeneo yenye mafuta yanayoweza kujaza mapipa bilioni tano hivi ndiyo makubwa zaidi, ilhali maeneo yenye kiasi cha mafuta kinachoweza kujaza mapipa milioni mia tano hadi bilioni tano ndiyo ya pili kwa ukubwa. Ingawa “Ripoti ya Marekani ya Nchi Zenye Mafuta Duniani ya Mwaka wa 2000” inaonyesha kwamba nchi 70 zina mafuta, ni chache tu zenye maeneo makubwa zaidi ya mafuta. (Ona sanduku kwenye ukurasa wa 7.) Maeneo makubwa zaidi ya mafuta yanapatikana hasa katika bonde la Arabuni na Iran, katika Ghuba ya Uajemi.

      Jitihada za kutafuta maeneo yenye mafuta hazijakoma. Badala yake, teknolojia mpya imeimarisha jitihada hizo. Kwa sasa, eneo la Bahari ya Caspian, linalotia ndani mataifa kama Azerbaijan, Iran, Kazakhstan, Turkmenistan, Urusi, na Uzbekistan, limevutia wachimbaji wa mafuta. Kulingana na Shirika la Marekani Linalosimamia Habari za Nishati, huenda mafuta na gesi ya asili yanapatikana katika eneo hilo. Njia nyingine za kusafirisha mafuta zinachunguzwa, kama vile kuyasafirisha kupitia Afghanistan. Pia kuna uwezekano kwamba kuna mafuta katika Mashariki ya Kati, Greenland, na maeneo fulani ya Afrika.

  • Mafuta Hutoka Wapi?
    Amkeni!—2003 | Novemba 8
    • [Grafu katika ukurasa wa 7]

      (Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

      SEHEMU ZENYE MAFUTA MENGI

      Idadi zinawakilisha mabilioni ya mapipa. Hazitii ndani mafuta ambayo hayajagunduliwa

      ▪ Mwanachama wa OPEC

      • Nchi yenye angalau eneo moja kubwa zaidi la mafuta

      Jumla ya uzalishaji

      ◆ Hifadhi

      ▪ • ◆ 332.7 SAUDI ARABIA

      • ◆ 216.5 MAREKANI

      • ◆ 192.6 URUSI

      ▪ • ◆ 135.9 IRAN

      ▪ • ◆ 130.6 VENEZUELA

      ▪ • ◆ 125.1 KUWAIT

      ▪ • ◆ 122.8 IRAKI

      ▪ • ◆ 113.3 MILKI ZA KIARABU

      • ◆ 70.9 MEXICO

      • ◆ 42.9 CHINA

      ▪ • ◆ 41.9 LIBYA

      ▪ ◆ 33.4 NIGERIA

      ◆ 21.2 KANADA

      ▪ ◆ 21.0 INDONESIA

      ◆ 20.5 KAZAKHSTAN

      ▪ • ◆ 18.3 ALGERIA

      ◆ 17.6 NORWAY

      ◆ 16.9 UINGEREZA

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki