-
Mafuta Hutoka Wapi?Amkeni!—2003 | Novemba 8
-
-
Mafuta Huchimbwaje?
Wanajiolojia na masoroveya hutafuta maeneo ambayo huenda yakawa na mafuta yasiyosafishwa ardhini. Baada ya kuchunguza na kuchukua sampuli, wao huchimba ili wahakikishe kwamba kuna mafuta. Zamani, kisima cha mafuta kilipochimbwa, mchanganyiko wa matope na mafuta ulitoka kwa nguvu na hivyo mafuta mengi yalipotea, na hata kungetokea mlipuko. Hata hivyo, mashine za kuchimba huzuia tatizo hilo kwa sababu zina vali za pekee na vifaa vya kupima. Leo pia inawezekana kuchimba visima vyembamba vyenye kina kirefu.
Hatimaye, mafuta na gesi huibuka kwa utaratibu na hali hiyo hudumishwa kwa kutia maji, kemikali, kaboni-dioksidi, na gesi nyingine kama nitrojeni. Mafuta yanaweza kuwa na uzito mbalimbali ikitegemea eneo. Kwa kawaida, mafuta mepesi yanapendwa sana kwa kuwa ni rahisi kuyachimba na kuyasafisha.
Taasisi ya Mafuta ya Marekani inasema kwamba teknolojia ya kisasa hutumiwa kuchimba mashimo ya mlalo, yaliyo sambamba na miamba ya dunia na hivyo si lazima kuchimba visima vingi. Uchimbaji wa mafuta baharini ulianza katika mwaka wa 1947 katika Ghuba ya Mexico na umeongeza kiasi cha mafuta. Hapana shaka kwamba njia inayotumiwa kuchimba mafuta huathiri bei yake.b
Mafuta Husafirishwaje?
Mnamo mwaka wa 1863, mabomba membamba ya mbao yalitengenezwa ili kusafirisha mafuta, kwa sababu yalipunguza gharama na yalikuwa rahisi kutumia kuliko mapipa ya lita 159 yaliyobebwa kwa magari yaliyokokotwa na farasi.c Leo mabomba mengi tata hutumiwa. Shirika la Mabomba ya Mafuta linasema kwamba mabomba yenye urefu wa kilometa 300,000 hutumiwa kusafirisha mafuta nchini Marekani pekee!
Mabomba, hasa ya chuma, husafirisha mafuta yasiyosafishwa hadi kwenye viwanda vya kusafisha na pia mafuta yaliyosafishwa hadi kwa wauzaji. Mabomba ya kisasa yanaweza kuwa na mifumo ya kompyuta inayochunguza mtiririko na msukumo wa mafuta. Vifaa vya kuchunguza mabomba kwa mamia ya kilometa, vifaa vinavyotumia nguvu za sumaku, na vifaa vinavyotumia mawimbi ya sauti kuchunguza mashimo kwenye mabomba vimebuniwa. Lakini, watu wanaotumia mafuta huona tu ishara inayoonyesha kwamba bomba la mafuta linapita ardhini na onyo la kuwatahadharisha wasilime sehemu hiyo.
Ingawa mabomba ni muhimu, si njia bora ya kusafirisha mafuta mengi katika nchi za mbali, na wauzaji wa mafuta wa hapo kale waliona inafaa kutumia meli kubwa za mafuta. Meli hizo huundwa kwa njia ya pekee na hufikia urefu wa meta 400 hivi. Meli za mafuta ndizo meli kubwa zaidi baharini na zinaweza kubeba mapipa milioni moja au zaidi ya mafuta. Lakini, zijapokuwa kubwa, meli za mafuta hukabili hatari ambayo haijashughulikiwa hadi sasa kama sanduku lenye kichwa “Kumwagika kwa Mafuta” linavyoonyesha. Mashua na magari ya moshi hutumiwa pia kwa ukawaida kusafirisha mafuta mengi. Hata hivyo, kusafirisha mafuta ni sehemu tu ya utaratibu wote wa uzalishaji.
Unaweza kutambua kiwanda cha kusafisha mafuta unapoona mwali mdogo wa moto ukiwaka juu ya mlingoti mrefu. Kwa kawaida mafuta yasiyosafishwa huchemshwa na kuelekezwa kwenye mnara wa kuvukiza, ambako hutenganishwa katika visehemu mbalimbali. Baadhi ya visehemu hivyo huwa vyepesi kama gesi ya butani, na vingine huwa vizito na hutumiwa kutengeneza mafuta ya kulainisha na bidhaa nyingine. (Ona ukurasa wa 8-9.)
-
-
Mafuta Hutoka Wapi?Amkeni!—2003 | Novemba 8
-
-
b “Inakadiriwa kwamba gharama ya uchimbaji wa mafuta kwa kutumia mnara uliojengwa zaidi ya meta 300 [futi 1,000] baharini katika Ghuba ya Mexico ni mara 65 hivi kuliko gharama ya uzalishaji huko Mashariki ya Kati.”—The Encyclopædia Britannica.
c Zamani, mafuta yalihifadhiwa na kusafirishwa kwa kutumia mapipa ya mbao kama yale yaliyotumiwa kwa ajili ya divai.—Ona sanduku kwenye ukurasa wa 5.
-
-
Mafuta Hutoka Wapi?Amkeni!—2003 | Novemba 8
-
-
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
UZALISHAJI WA MAFUTA MAELEZO SAHILI
1—KUPIMA
SATELAITI
Mfumo wa Kupokea Habari Kutoka kwa Satelaiti hutoa ishara sahihi ambazo hutumiwa katika uchunguzi
VIKUZA-SAUTI
MALORI YANAYOELEKEZA MAWIMBI YA SAUTI ARDHINI
MELI ZINAZOELEKEZA MAWIMBI YA SAUTI BAHARINI
MABOMBA
Njia moja ni kupima mwangwi wa sauti inayoelekezwa ardhini
2—KUCHIMBA
VISIMA VYA NCHI KAVU
JUKWAA LA BAHARINI
KISIMA KILICHO MAJINI
Visima vya mafuta huchimbwa katika nchi kavu, karibu na ufuo, na chini ya bahari. Huenda gesi au kemikali zikatiwa kisimani ili kudumisha msukumo wa mafuta
[Picha]
KISIMA KILICHO MAJINI
Nyambizi zinazoendeshwa kutoka mbali hutumiwa kujenga vifaa vya uzalishaji chini ya bahari
[Picha]
KUCHIMBA KISIMA CHA MLALO
Mashine zinazoendeshwa kutoka mbali na mtaalamu huzungusha mtaimbo wa kuchimba, na vifaa maalumu huchunguza mwamba
3—KUSAFIRISHA
MELI YA MAFUTA
Mafuta husafirishwa kwa mabomba yaliyo juu ya ardhi, chini ya ardhi, na baharini. Mafuta husafirishwa pia kwa meli, mashua, na magari ya moshi
4—KUSAFISHA
MTAMBO WA KUSAFISHA
Mafuta yasiyosafishwa huchemshwa, huvukizwa, na kutenganishwa katika visehemu vinavyoweza kutumiwa kutengeneza bidhaa mbalimbali
MNARA WA KUVUKIZA
Mafuta meusi yasiyosafishwa yanayonata huchemshwa katika tanuru, kisha haidrojeni na kaboni huyeyuka na kuwa gesi. Gesi hizo hubadilika na kuwa majimaji katika vipimo mbalimbali vya joto. Hivyo mafuta hutenganishwa katika visehemu kadhaa
68°F. → GESI ZA KUSAFISHA Zinatia ndani methani, ethani,
[20°C] propani, na butani
↑ ↑
70°-160°F. → PETROLI Hutumiwa kuendesha magari na
[20°-70°C] kutengeneza plastiki
↑ ↑
160°-320°F. → NAFTHA Inaweza kutumiwa kutengeneza
[70°-160°C] plastiki, petroli, na kemikali
nyingine
↑ ↑
320°-480°F. → MAFUTA YA TAA Hutengeneza mafuta ya ndege na [160°-250°C] hutumiwa katika jiko la mafuta oil
↑ ↑
480°-660°F. → MAFUTA YA GESI Hutengeneza dizeli na mafuta ya tanuru
[250°-350°C]
↑ ↑
750°F. → MABAKI Hutumiwa kutengeneza mafuta ya
↑ ↑ kusafisha, mafuta mazito, nta ya
mishumaa, grisi, na lami
TANURU
MTAMBO WA KUYEYUSHA WENYE KICHOCHEZI
Haidrojeni na kaboni huchomwa kwa mvuke na kuchanganywa na kichochezi moto cha mchanganyiko wa ungaunga wa alumini na silika. Haidrojeni na kaboni huvunjwa na kufanyiza molekuli ndogo muhimu
Kichochezi cha ungaunga huchanganyika na haidrojeni na kaboni katika mvuke
ETHANOLI
Kiyeyusho hiki hutumiwa kutengeneza rangi, vipodozi, marashi, sabuni, na rangi za nguo
PLASTIKI
Kwa mfano, polisterini hutengenezwa kwa kuunganisha molekuli nyingi za sterini
NYONGEZA ZA PETROLI
Oktani huzuia gesi isiwake haraka sana kwenye injini, na hivyo injini hufanya kazi vizuri zaidi
[Hisani]
-