Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuimba Wimbo Mpya wa Sherehe ya Ushindi
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Tayari, Ufunuo 7:1, 3 umetufumbulia kwamba pepo nne za uharibifu zinazuiwa mpaka wote 144,000 wa hawa watumwa wapakwa-mafuta waishe kutiwa muhuri. Ufunuo 12:17 umejulisha kwamba hawa “wabakio wa mbegu [ya mwanamke]” wanakuwa shabaha ya pekee ya Shetani, drakoni, katika wakati huo. Na Ufunuo 13 umeonyesha picha iliyo wazi ya matengenezo ya kisiasa ambayo Shetani ameinua duniani ili kuleta mbano mwingi na mnyanyaso wa ukatili juu ya watumishi waaminifu wa Yehova. Lakini adui mkuu huyo hawezi kubatili kusudi la Mungu! Sasa tutajifunza kwamba ujapokuwa utendaji wa nia mbovu wa Shetani, 144,000 wote wanakusanywa kwa ushindi wenye shangwe.

  • Kuimba Wimbo Mpya wa Sherehe ya Ushindi
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 4. Inakuwaje kwamba 144,000 wote wanasimama juu ya Mlima Sayuni?

      4 Yohana anaona Yesu na pia mwili kamili wa 144,000 warithi wenzi wa Ufalme wa kimbingu wakiwa wanasimama juu ya Mlima Sayuni. Katika wakati unaowakilishwa na njozi, wengi, lakini si wote, wa wale 144,000 tayari wako katika mbingu. Baadaye katika njozi iyo hiyo, Yohana anajifunza kwamba baadhi ya watakatifu wangali wanapaswa kuvumilia na kufa wakiwa waaminifu. (Ufunuo 14:12, 13) Kwa wazi, basi, baadhi ya 144,000 wangali wako duniani. Kwa hiyo inakuwaje kwamba Yohana anaona 144,000 wote wakisimama pamoja na Yesu juu ya Mlima Sayuni?a Kwamba, wakiwa washiriki wa kundi la Wakristo wapakwa-mafuta, sasa hawa ‘wamekaribia Mlima Sayuni na jiji la Mungu aliye hai, Yerusalemu la kimbingu.’ (Waebrania 12:22, NW) Kama Paulo wakati alipokuwa angali duniani, tayari wao—katika maana ya kiroho—wameinuliwa juu wakawe katika muungano na Kristo Yesu katika mahali pa kimbingu. (Waefeso 2:5, 6) Kwa kuongezea, katika 1919 wao waliitikia mwito, “Njooni juu huku,” na kitamathali ‘walienda ndani ya mbingu katika wingu.’ (Ufunuo 11:12, NW) Kwa sababu ya maandiko haya, sisi tunaweza kuona kwamba wote 144,000—kusema kiroho—wako kwenye Mlima Sayuni pamoja na Yesu Kristo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki