Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuimba Wimbo Mpya wa Sherehe ya Ushindi
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 14. (a) Ni jinsi gani 144,000 ni “matunda ya kwanza kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo”? (b) Ni katika maana gani umati mkubwa pia ni matunda ya kwanza?

      14 Hao 144,000 ‘hununuliwa kutoka dunia,’ ‘hununuliwa kutoka miongoni mwa aina ya binadamu.’ Wao wanalelewa kuwa wana wa Mungu, na baada ya ufufuo wao, hawatakuwa tena binadamu tu wa mnofu na damu. Kama inavyotajwa katika mstari wa 4, wao wanakuwa “matunda ya kwanza kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.” Kweli, huko nyuma katika karne ya kwanza, Yesu alikuwa “matunda ya kwanza kwa wale ambao wamelala usingizi katika kifo.” (1 Wakorintho 15:20, 23, NW) Lakini 144,000 ni “matunda ya kwanza fulani” ya aina ya binadamu wasiokamilika, walionunuliwa kwa dhabihu ya Yesu. (Yakobo 1:18, NW)

  • Kuimba Wimbo Mpya wa Sherehe ya Ushindi
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Katika siku ya 50 kutoka Nisani 16, katika mwezi wa tatu, Waisraeli walisherehekea siku ya vuno la matunda mapevu ya kwanza ya vuno la ngano. (Kutoka 23:16; Walawi 23:15, 16) Sikukuu hii ikaja kuitwa Pentekoste (Kutokana na neno la Kigiriki linalomaanisha “-a hamsini”), na ilikuwa kwenye Pentekoste 33 W.K. kwamba washiriki wa kwanza wa 144,000 wakapakwa mafuta kwa roho takatifu.

  • Kuimba Wimbo Mpya wa Sherehe ya Ushindi
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Hawa walinunuliwa kutoka miongoni mwa aina ya binadamu wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo,

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki