-
Sydney—Jiji la Bandari Lenye PilikapilikaAmkeni!—1999 | Julai 8
-
-
Kito cha Sydney Kwenye Bandari
Jumba la Opera la Sydney limeitwa “kito cha Bennelong Point,” nalo limezingirwa kwenye pande tatu na maji ya samawati ya Bandari ya Sydney. Kwa kweli jumba hilo hufanana na kito kwenye jua jangavu. Wakati wa usiku magamba yake ya kikale hung’aa kabisa kwenye taa za jumba hilo la opera.
Dibaji ya kitabu A Vision Takes Form hufafanua jinsi mtu huvutiwa anapoona jumba la opera: “Jumba la Opera la Sydney limekuwa mojawapo ya majengo ambayo hubadilika-badilika kulingana na mahali alipo mtu na kulingana na badiliko la nuru. . . . Ukungu wa asubuhi au mionzi ya jua ya jioni zaweza kuangaza magamba yake ili yafanane na kofia kubwa za majitu kwenye hadithi za hekaya.”
Michoro ya jumba hilo la opera ilifanyizwa na msanifuujenzi wa Denmark Jørn Utzon na hatimaye uliteuliwa katika mashindano ya uchoraji miongoni mwa zaidi ya michoro 200 iliyotoka mataifa mbalimbali. Lakini ilionekana haiwezekani kutumia sehemu fulani-fulani za michoro yake nazo zikabadilishwa sana.
Gazeti Architects’ Journal la London lilitaja mchoro huo kuwa “upeo wa ubuni wenye kuvutia sana ulio mkubwa sana.” Lakini, kujenga kwenyewe kutokana na wazo hilo kulikuwa jambo gumu sana kwa wahandisi. Wahandisi wawili, Sir Ove Arup na Jack Zunz, walisema: “Jumba la Opera la Sydney ni . . . mwito mkubwa sana wa ujenzi. . . . Kwa sababu linajengwa chini ya hali zisizo za kawaida kabisa, na kwa vile lina matatizo makubwa sana, limetokeza hali za kipekee . . . za kukuza mbinu mpya. Nyingi za mbinu hizo tayari zimetumiwa katika madaraja ya kawaida na majengo mengi.”
Kadirio la awali la gharama ya jumba la opera lilikuwa dola milioni 7 za Australia, lakini kufikia wakati lilipomalizika mwaka wa 1973, gharama hiyo ilikuwa imeruka kufikia dola milioni 102!
Jinsi Jumba la Opera Linavyofanana Ndani
Tuingiapo sebuleni, twaona kwamba nuru ya jua yapitia tabaka mbili za kioo kwenye midomo ya yale magamba. Jumba hilo limezingirwa kwa kioo cha kipekee kilichotengenezwa Ufaransa chenye jumla ya meta 6,225 za mraba. Kisha twaingia ndani ya ukumbi wa michezo. Tunapokuwa tumesimama upande wa nyuma tukitazama viti 2,690 vinavyoelekea jukwaa, twashangaa kuona kinanda kiitwacho tracker organ kinachoendeshwa na mashine ambacho ndicho kikubwa zaidi ulimwenguni, kikiwa na zumari 10,500.a Dari yafikia meta 25 kutoka chini ikifanya ukumbi uwe na uwezo wa meta 26,400 za kyubiki. Jambo hilo “hufanya kuwe na mwangwi kwa karibu sekunde mbili na kuruhusu muziki wenye kupatana usikike kikamili zaidi,” yasema broshua moja rasmi ya mwongozo.
Kumbi nyinginezo tatu zinavutia vilevile, nazo zilikusudiwa kwa ajili ya opera, maonyesho ya muziki, dansi aina ya ballet, sinema, kukariri mashairi, drama, muziki wa ala, maonyesho, na mikusanyiko. Kuna jumla ya vyumba 1,000 katika jumba la opera, kutia ndani mikahawa, vyumba vya kubadilishia mavazi, na vyumba vya mambo mengine.
-
-
Sydney—Jiji la Bandari Lenye PilikapilikaAmkeni!—1999 | Julai 8
-
-
[Picha katika ukurasa wa 16, 17]
Jumba la Opera la Sydney pamoja na daraja la bandari
[Picha zimeandiliwa na]
By courtesy of Sydney Opera House Trust (photograph by Tracy Schramm)
[Picha katika ukurasa wa 17]
Ndani ya Jumba la Opera, likiwa na kinanda chenye zumari 10,500
[Picha zimeandilwa na]
By courtesy of Australian Archives, Canberra, A.C.T.
-