Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kwa Nini Nitunze Afya Yangu?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
    • Kula Vizuri​—Uwe na Afya Nzuri!

      Biblia inatuhimiza tuwe na kiasi katika mazoea yetu. “Usiwe mwenye . . . kujishindilia chakula,” yasema Methali 23:20. (Contemporary English Version) Nyakati nyingine, si rahisi kufuata shauri hilo.

      “Sawa na vijana wengi, mimi huwa na njaa kila wakati. Wazazi wangu husema tumbo langu ni shimo lisilo na mwisho!”—Andrew, mwenye umri wa miaka 15.

      “Kwa kuwa siwezi kuelewa jinsi vyakula fulani vinavyonidhuru kwa sasa, sioni vikiwa vibaya sana hivyo.”—Danielle, mwenye umri wa miaka 19.

      Je, unahitaji kujizuia zaidi kuhusiana na mazoea yako ya kula? Yafuatayo ni mambo ambayo vijana wenzako wanasema yamewasaidia.

      Sikiliza tumbo lako. “Nilikuwa nikihesabu kalori,” asema Julia, mwenye umri wa miaka 19, “lakini sasa ninapoanza kuhisi nimeshiba, ninaacha kula.”

      Epuka vyakula visivyo na lishe. “Nilipoacha kunywa soda,” asema Peter, mwenye umri wa miaka 21, “nilipunguza uzito wangu kwa kilo tano baada ya mwezi mmoja tu!”

      Epuka mazoea mabaya ya kula. “Mimi hujaribu sana kutoongeza chakula,” asema Erin, mwenye umri wa miaka 19.

      Siri ya Kufanikiwa: Usikose-kose milo! Ukifanya hivyo, utakuwa na njaa nawe huenda ukashawishika kula chakula kingi zaidi.

  • Kwa Nini Nitunze Afya Yangu?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
    • [Sanduku katika ukurasa wa 73]

      “Nilibadili Maisha Yangu”

      “Nilipokuwa tineja, nilikuwa mnene kupita kiasi, jambo ambalo halikunipendeza kamwe. Nilihuzunishwa sana na jinsi nilivyoonekana na kuhisi! Mara kwa mara nilijaribu kupunguza uzito wangu kwa kula vyakula maalumu, lakini muda si muda nilianza kunenepa tena. Kwa hiyo, nilipokuwa na umri wa miaka 15, niliamua imetosha. Niliamua kupunguza uzito kwa njia inayofaa—njia ambayo ningeweza kudumisha katika maisha yangu yote. Nilinunua kitabu kinachozungumzia kanuni za msingi za lishe bora na jinsi ya kufanya mazoezi, nami nikaanza kutumia habari hizo maishani mwangu. Niliazimia kwamba hata nikiteleza na kuanguka au kuvunjika moyo, sitakata tamaa. Wajua nini? Nilifaulu! Baada ya mwaka mmoja, nilipunguza kilo 27. Nimedumisha uzito huo kwa miaka miwili. Sikufikiri kamwe kwamba ningeweza kufaulu! Nafikiri sababu hasa ya kufaulu kwangu si chakula fulani maalumu, bali kwamba nilibadili maisha yangu.”—Catherine, mwenye umri wa miaka 18.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki