Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mizizi ya Krismasi ya Kisasa
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Desemba 15
    • Kufikia katikati ya karne ya nne, kuguna kwa wapagani kulitulia. Jinsi gani? Wakristo bandia zaidi na zaidi walipopenya ndani ya kundi, mawazo ya uasi-imani yalizidi. Jambo hilo liliongoza kwenye kuridhiana na ulimwengu wa Roma. Kikieleza juu ya hilo, kitabu The Paganism in Our Christianity chataarifu hivi: “Ilikuwa ni sera hususa ya Kikristo kuidhibiti na kuipa umaana wa Kikristo misherehekeo ya kipagani ambayo pokeo lilifanya ipendwe na watu.” Ndiyo, uasi-imani mkubwa ulikuwa ukitokeza madhara yake. Utayari wa wale waitwao Wakristo isivyofaa wa kukubali rasmi sherehe za kipagani sasa ulileta kiasi fulani cha ukubalifu ndani ya jumuiya. Punde si punde, Wakristo walipata kuwa na misherehekeo mingi ya kila mwaka kama vile wapagani wenyewe. Haishangazi kwamba Krismasi ilikuwa ya kwanza kabisa miongoni mwa hiyo misherehekeo.

  • Mizizi ya Krismasi ya Kisasa
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Desemba 15
    • Upesi Krismasi ilitwaa sehemu nyingi kutoka misherehekeo ya mavuno ya kilimwengu ya Kaskazini mwa Ulaya. Kusherehekea kuliendelea kuwa kwa kawaida zaidi ya uchaji kwa maana washerehekeaji walijitia mno katika ulafi na ulevi. Badala ya kuteta dhidi ya mwenendo mlegevu, kanisa liliukubali. (Linganisha Waroma 13:13; 1 Petro 4:3.) Mwaka wa 601 W.K., Papa Gregory wa Kwanza alimwandikia Mellitus, mmishonari wake huko Uingereza, akimwambia “[asi]komeshe shughuli hizo za sherehe za kipagani, lakini kuzirekebisha zifae sherehe ya ibada ya Kanisa, kubadili tu sababu ya sherehe hizo kuwa msukumo wa Kikristo bali si wa kipagani.” Hivyo ndivyo aripotivyo Arthur Weigall, aliyekuwa wakati mmoja mkaguzi mkuu wa mambo ya kale wa serikali ya Misri.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki