Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Mungu wa Pekee wa Kweli” Ni Nani?
    Amkeni!—2005 | Aprili 22
    • Chanzo cha Utatu

      Biblia inataja kwamba kuna miungu mingi inayoabudiwa na watu, kutia ndani Ashtorethi, Milkomu, Kemoshi, na Moleki. (1 Wafalme 11:1, 2, 5, 7) Hata watu wengi katika taifa la kale la Israeli wakati mmoja waliamini kwamba Baali ndiye Mungu wa kweli. Kwa hiyo, Eliya, nabii wa Yehova akawaambia hivi: “Ikiwa Yehova ndiye Mungu wa kweli, mfuateni yeye; lakini ikiwa ni Baali, mfuateni yeye.”—1 Wafalme 18:21.

      Kabla ya Yesu kuzaliwa, wapagani walizoea kuabudu miungu mitatu-mitatu. Mwanahistoria Will Durant anasema: “Dhana za utatu mtakatifu zilianzia Misri.” Katika kichapo kimoja (Encyclopædia of Religion and Ethics) James Hastings aliandika: “Kwa mfano, katika dini ya Kihindi kuna miungu watatu: Brahmā, Siva, na Viṣṇu; na katika dini ya Misri kuna miungu watatu Osiris, Isis, na Horus.”

  • “Mungu wa Pekee wa Kweli” Ni Nani?
    Amkeni!—2005 | Aprili 22
    • [Picha katika ukurasa wa 7]

      MISRI

      Utatu wa Horus, Osiris, na Isis, katika milenia ya pili K.W.K.

      [Picha katika ukurasa wa 7]

      PALMYRA, SYRIA

      Utatu wa mungu mwezi, Bwana wa Mbingu, na mungu jua, karne ya kwanza hivi W.K.

      [Picha katika ukurasa wa 7]

      INDIA

      Utatu wa mungu wa Kihindu, karne ya saba hivi W.K.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki