-
Kuokolewa Kutoka Kwenye Dhoruba Yenye Kufisha!Amkeni!—1999 | Juni 8
-
-
Akina ndugu katika Panama walisimamisha vituo vinne vya kupokea, kuchagua, na kupakia vitu vilivyotolewa. Katika siku chache, misaada inayozidi kilogramu 20,000 ilikuwa imekusanywa. Mtu mmoja asiyekuwa Shahidi alisema hivi: “Nilifikiri kwamba majeshi ndiyo yaliyokuwa namba moja katika kupanga kazi ya kutoa msaada. Lakini sasa ninaona Mashahidi wa Yehova ndio wa kwanza.” Sasa Mashahidi wameanza kumtembelea mtu huyo kwa ukawaida ili kushiriki naye kweli za Biblia.
Ndugu mmoja anayefanya kazi katika shirika la usafiri alitoa trela ndogo na dereva (asiyekuwa Shahidi) kupeleka misaada huko Nikaragua. Maofisa katika Panama na Kosta Rika hawakudai ushuru wa forodha waliporuhusu lori hilo lipite kwenye mipaka yao. Kituo kimoja cha petroli kilitoa fueli ya kutosha kujaza matangi yote mawili ya lori hilo—iliyotosha safari ya kwenda na kurudi! Katika Nikaragua maofisa wa forodha vilevile hawakukagua vifurushi hivyo. “Ikiwa vitu hivi vinatoka kwa Mashahidi wa Yehova, hatuhitaji kuvikagua,” wakasema. “Hawatusumbui kamwe.”
-
-
Kuokolewa Kutoka Kwenye Dhoruba Yenye Kufisha!Amkeni!—1999 | Juni 8
-
-
Wafanyakazi wa uwanja wa ndege katika Panama walivutiwa hasa kuona zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea 20 waliokuwa Mashahidi wakisaidia kupakua misaada iliyotolewa kupelekwa Honduras. Siku iliyofuata, baadhi ya wafanyakazi hawa wa uwanja wa ndege walijitokeza wakiwa na michango waliyokuwa wamekusanya miongoni mwao wenyewe.
-