Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mkutano Uliokazia Umoja na Kuzungumzia Mipango Yenye Kusisimua
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 15
    • RIPOTI NZURI KUTOKA MEXICO

      Sehemu ya kwanza ya programu ilionyesha umoja uliopo miongoni mwa watu wa Yehova. Baltasar Perla aliwahoji washiriki wenzake watatu wa familia ya Betheli ya Mexico kuhusu kuunganishwa kwa ofisi sita za tawi katika bara la Amerika ya Kati na ofisi ya tawi ya Mexico. Kwa sababu ya kuunganishwa kwa ofisi hizo, sasa familia ya Betheli ya Mexico ina washiriki wengi zaidi kutoka katika tamaduni na nchi mbalimbali. Ongezeko hilo la waamini wenzetu kutoka katika nchi mbalimbali limetokeza badilishano la kitia-moyo. Ni kana kwamba Mungu alichukua kifutio kikubwa na kufuta kabisa mipaka ya kitaifa.

      Changamoto moja iliyosababishwa na kuunganishwa kwa ofisi hizo ilikuwa kuwasaidia wahubiri kutohisi kwamba wako mbali sana na tengenezo la Yehova hata ingawa ofisi za tawi zimefungwa katika nchi zao. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, kila kutaniko linawasiliana na ofisi ya tawi kupitia barua-pepe iliyo salama na kwa njia hiyo hata makutaniko ya mashambani yanaweza kuwasiliana moja kwa moja na ofisi ya tawi.

  • Mkutano Uliokazia Umoja na Kuzungumzia Mipango Yenye Kusisimua
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 15
    • PANAMA

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki