Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • KUKABILIANA NA MADHEHEBU YA WAABUDU-MALI

      Mnamo 1960, mapainia wa pekee wengine wawili kutoka Australia, Stephen Blundy na Allen Hosking, walihamia kijiji cha Savaiviri kilichoko kilomita 50 hivi mashariki ya Kerema. Baada ya kuishi katika hema kwa miezi mitatu, Stephen na Allen walihamia katika nyumba ndogo ya msituni iliyokuwa katika shamba la minazi lililozungukwa na kinamasi kikubwa.

      Savaiviri lilikuwa eneo linalojulikana sana kwa sababu ya madhehebu yake ya waabudu-mali. Madhehebu hiyo ilianza jinsi gani? Wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu, wenyeji walistaajabishwa na utajiri, au mali, ambazo askari-jeshi wageni walikuwa nazo. Kisha vita vilikwisha, na wanajeshi wakafunga virago vyao na kuondoka. Wanakijiji fulani walisema kwamba kwa kuwa mali hizo zilikuwa zimetoka mbali sana mahali wasipoweza kuona—kwa kuwa wanaamini kuwa pepo wanaishi mahali pasipoonekana—basi mababu zao waliokufa walikuwa wakiwatumia mali hizo lakini wanajeshi hao ndio waliokuwa wakizuia. Ili kuwajulisha pepo uhitaji wao, watu waliigiza vita na kujenga gati zenye nguvu ili kujitayarishia kwa ajili ya siku hiyo tukufu wakati ambapo mali mpya zingefika.

      Baada ya muda, Stephen na Allen walikuwa wakijfunza na washiriki 250 hivi wa madhehebu hiyo, kutia ndani kiongozi wao na baadhi ya “mitume kumi na wawili” wake. “Wengi kati ya watu hao walikubali kweli,” anasema Stephen. “Kwa kweli, ofisa mmoja wa serikali alituambia baadaye kwamba kazi yetu ya kuhubiri iliwasaidia sana kumaliza madhehebu hiyo ya waabudu-mali huko Savaiviri.”

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 97]

      Stephen Blundy akivuka Ghuba ya Kerema

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki