Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • “Katika nchi iliyo na zaidi ya lugha 800, ni muhimu kuwa na lugha moja au zaidi ambazo watu wanaweza kutumia kuwasiliana,” anasema Timo Rajalehto, ambaye ni mshiriki wa Halmashauri ya Tawi na msimamizi wa Idara ya Tafsiri. “Lugha rahisi zinazotumiwa katika biashara, kama vile Kitok Pisin na Kihiri Motu zinafaa kwa kusudi hilo. Ni rahisi kujifunza lugha hizo, na pia zinatumiwa katika shughuli za kila siku. Lakini haziwasilishi kwa njia inayofaa hoja ngumu. Kwa hiyo, mara nyingi watafsiri wetu hushindwa kueleza maneno mengine magumu.

      “Kwa mfano, tuligundua kwamba hakuna neno la Kitok Pisin linaloweza kutafsiri kwa kufaa neno ‘kanuni.’ Kwa hiyo, watafsiri wetu waliunganisha maneno mawili ya lugha ya Tok Pisin ili kufanyiza neno stiatok (maneno ya kuelekeza), ambalo hufafanua jinsi ambavyo kanuni zinafanya kazi kwa kuwaelekeza watu katika njia inayofaa. Neno hilo lilianza kutumiwa na vyombo vya habari na sasa linatumiwa na watu wengi wanaozungumza Kitok Pisin.”

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • “Hivi majuzi, tulitafsiri baadhi ya trakti katika lugha mpya, kutia ndani lugha ya Enga, Jiwaka, Kuanua, Melpa, na Orokaiva,” anasema Timo Rajalehto. “Kwa kuwa watu wanaozungumza lugha hizo huzungumza pia lugha ya Tok Pisin au Kiingereza, au lugha zote mbili, kwa nini hilo lilifanywa? Tulitaka kuona jinsi ambavyo watu wataitikia ujumbe wa Ufalme katika lugha yao ya kienyeji. Je, watavutiwa na kweli na wawe na maoni yanayofaa kuwaelekea Mashahidi?

      “Jibu la wazi ni ndiyo! Kwa kweli, kumekuwa na maelezo mengi mazuri kuhusu jambo hilo. Mafunzo ya Biblia yameanzishwa, na hata watu fulani ambao hapo awali walitupinga wamebadili mtazamo wao kuwaelekea Mashahidi. Watu wanapopata kichapo katika lugha yao ya kienyeji, jambo hilo huwa na matokeo mazuri.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki