-
Papua New Guinea2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Baadaye, Jim Wright, mwana wa Dorothy, pamoja na painia mwenzake, Kerry Kay-Smith walipewa mgawo wa kwenda Banz, wilaya ya kukuza chai na kahawa katika bonde maridadi la Wahgi mashariki ya Mlima Hagen. Huko walikabili upinzani mkali kutoka kwa makanisa, ambayo yaliwachochea watoto wawatupie mawe na kuwafukuza kutoka vijijini mwao.
-
-
Papua New Guinea2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
“Wakati wa kusanyiko hilo, nilihojiwa jukwaani na nikaeleza mateso ambayo tulivumilia zamani huko Banz,” akasema Jim. “Karibu kila mtu aliyekuwa akisikiliza alitokwa na machozi. Baada ya programu baadhi ya akina ndugu walikuja wakanikumbatia na kuomba msamaha huku wakitokwa na machozi. Walipokuwa wavulana, walikuwa wamenifukuza kutoka kijijini mwao huku wakinitupia mawe na kunitusi. Isitoshe, mmoja wao, Mange Samgar—ambaye sasa ni mzee—ndiye kasisi wa Kilutheri aliyekuwa amewachochea wafanye hivyo! Kusanyiko hilo lilikuwa wakati mzuri kama nini wa kukutana tena!”
-