-
Papua New Guinea2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
WATOTO WANAOMLETEA SIFA MUUMBA WAO
Kwa kufuata kwa ujasiri dhamiri zao zilizozoezwa na Biblia, watoto wengi huko Papua New Guinea wametoa ushahidi mzuri. Kwa mfano, mapema katika mwaka wa 1966, mwalimu mmoja wa shule ya msingi aliwaambia watoto saba wa Mashahidi wa eneo hilo kwamba walipaswa kusalimu bendera wakati wa sherehe ambazo zingefanywa juma lililofuata. Siku hiyo ilipofika, watoto wote saba walikataa kusalimu bendera mbele ya wanafunzi 300 hivi. Kwa sababu hiyo, walifukuzwa shuleni, hata ingawa wazazi wao walikuwa wameandika barua wakiomba watoto wao wasihusishwe katika sherehe hizo. Mzee mmoja kutoka kutaniko la huko aliandika barua kwa maofisa wa serikali huko Papua New Guinea na Australia kuhusu jambo hilo.
Mnamo Machi 23, Msimamizi wa Serikali ya Australia huko Papua New Guinea aliwapigia simu wakuu wa shule hiyo na kuagiza kwamba watoto hao warudishwe shuleni mara moja. Ibada ya kweli ilikuwa imepata ushindi mdogo wa kisheria. Leo, serikali ya Papua New Guinea inaendelea kuheshimu haki ya watoto ya kukataa kusalimu bendera kwa sababu ya dhamiri.
-
-
Papua New Guinea2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 145]
Baadhi ya watoto waliofukuzwa shuleni kwa kukataa kusalimu bendera
-