Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Wakati huohuo, katika eneo jirani la Bulolo, Wally na Joy Busbridge walihubiri kwa bidii hivi kwamba wasimamizi wa Misheni ya Makabila Mapya wakakasirika, kwa kuwa waliona eneo hilo kuwa miliki yao. Kwa sababu ya kushinikizwa na kanisa hilo, mwajiri wa Wally alimwambia, “Uache dini yako, au utafute kazi nyingine.”

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Popondetta, mji mdogo ulio kusini-mashariki ya Lae, ulihubiriwa habari njema na Jerome na Lavinia Hotota ambao walirudi kwenye mkoa wa nyumbani kwao kutoka Port Moresby. Jerome alikuwa na bidii sana na alitumia Maandiko kwa ushawishi, naye Lavinia alikuwa mwanamke mwenye fadhili ambaye alipendezwa sana kibinafsi na wengine. Kama ilivyotarajiwa, walipoanza tu kuhubiri askofu Mwanglikana pamoja na wengi wa wafuasi wake walifika nyumbani kwao na kuwaambia waache. Lakini Jerome na Lavinia hawakutishika.

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Kufikia mwaka wa 1963, habari njema ilikuwa imehubiriwa hadi Wewak, mji ulio mbali kwenye pwani ya kaskazini ya Papua New Guinea. Karl Teynor na Otto Eberhardt, wajenzi wawili Wajerumani, walijenga hospitali ya Wewak mchana na wakajifunza na zaidi ya watu 100 wakati wa jioni na miisho ya juma. Kazi yao ya kuhubiri ilimkasirisha sana kasisi Mkatoliki wa eneo hilo hivi kwamba akakusanya umati wenye ghasia na kutupa pikipiki za Karl na Otto baharini. Mtu mmoja aliyeshirikiana na kasisi huyo, kiongozi mashuhuri wa kijiji, alikuwa na mwana ambaye baadaye alikuja kuwa Shahidi. Kwa sababu ya kuvutiwa na mabadiliko aliyoona katika maisha ya mwana wake, mtazamo wa mtu huyo ulibadilika naye akawaruhusu Mashahidi wahubiri katika vijiji vilivyokuwa chini ya udhibiti wake.

  • Papua New Guinea
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • ‘WAPIGENI MARUFUKU MASHAHIDI’

      Wapinzani wetu hawakufurahia maendeleo hayo. Kuanzia 1960 na kuendelea, muungano wa makanisa yanayodai kuwa ya Kikristo, shirika la kuwategemeza wanajeshi waliostaafu na wanajeshi wengine wa Australia (Returned Services League, RSL), na vyombo vya habari vilianza kampeni iliyopangwa ya kuwavunjia heshima na kuwapiga marufuku Mashahidi wa Yehova.

      Mambo yalifikia kilele wakati ambapo karatasi iliyochapishwa kuhusu msimamo wetu juu ya kutiwa damu mishipani iliposambazwa kwa madaktari, makasisi, na maofisa wa serikali. Kama kawaida, makasisi wa dini zinazodai kuwa za Kikristo ndio waliokuwa wa kwanza kusema. Agosti 30, 1960, gazeti South Pacific Post lilikuwa na kichwa “Makanisa Yakasirishwa na Suala la Damu.” Katika makala inayokuwa ndani, viongozi wa kanisa walisema kuwa Mashahidi ni “wapinga-Kristo [na] maadui wa Kanisa.”

      Makala zilizofuata zilidai kwa uwongo kwamba Mashahidi wa Yehova ni wachochezi na kwamba mafundisho yao yaliwachochea watu wasiende shuleni, wasilipe kodi, wajiunge na madhehebu ya waabudu-mali, na wasidumishe usafi. Ripoti nyingine za uwongo ziliwashtaki kwa kutumia vibaya kupatwa kwa jua ili kuwaogopesha na “kuwadhibiti wenyeji wasio na elimu.” Gazeti moja hata liliwazomea Mashahidi kwa “kuishi, kula, na kufanya kazi pamoja na wanakijiji.” Gazeti South Pacific Post liliwachambua kwa kufundisha kwamba “watu wote wako sawa” na likadai kwamba Mashahidi ni “tisho kubwa kuliko Ukomunisti.”

      Mwishowe, Machi 25, 1962, RSL iliwaomba wenye mamlaka wakoloni wawapige Mashahidi marufuku. Hata hivyo, serikali ya Australia ilikataa waziwazi ombi hilo. “Tangazo hilo lilikuwa na matokeo mazuri katika nchi yote,” anasema Don Fielder. “Watu wenye akili zilizofunguka wangeweza kuona kwamba madai ya wapinzani hayakuwa ya kweli.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki