-
Je, Wajua?Mnara wa Mlinzi—2009 | Machi 1
-
-
“Wana wa Zeu” ambao wanatajwa katika Matendo 28:11 walikuwa nani?
Kitabu cha Biblia cha Matendo kinasema kwamba mtume Paulo alipokuwa akielekea Roma, alisafiri kutoka Malta hadi Puteoli kwa mashua iliyokuwa na sanamu ya gubeti ya “Wana wa Zeu.” (Matendo 28:11) Sanamu hizo za “Wana wa Zeu” zilitumiwa sana na mabaharia na wasafiri wa kale.
Kulingana na hadithi za Wagiriki na Waroma, Zeu (anayejulikana pia kama Sumbula) na Leda walikuwa na wana mapacha, walioitwa Castor na Pollux. Hao “Wana wa Zeu” walionwa kuwa mabaharia stadi waliokuwa na uwezo wa kudhibiti upepo na mawimbi. Hivyo, waliabudiwa kama miungu iliyowalinda mabaharia. Mabaharia waliwatolea dhabihu na kuwaomba wawalinde wakati wa dhoruba. Iliaminiwa kwamba miungu hiyo pacha ilionyesha nguvu zao za kulinda kupitia moto wa Mtakatifu Elmo. Nyakati nyingine moto huo ulionekana kwenye milingoti ya meli kulipokuwa na dhoruba.
Ibada ya Castor na Pollux ilikuwa imeenea sana kati ya Wagiriki na Waroma, na kitabu kimoja cha kale kinataja hasa ibada hiyo katika wilaya zilizozunguka Kirene, huko Afrika Kaskazini. Mashua inayotajwa katika kitabu cha Matendo ilikuwa imetoka karibu na eneo hilo, katika jiji la Aleksandria, huko Misri.
-
-
Je, Wajua?Mnara wa Mlinzi—2009 | Machi 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 9]
Sarufu ya Dinari yenye picha ya “Wana wa Zeu,” 114-113 K.W.K.
-