-
Ukristo Waenea Miongoni mwa Wayahudi wa Karne Ya KwanzaMnara wa Mlinzi—2005 | Oktoba 15
-
-
[Chati katika ukurasa wa 14]
HANGAIKO LA MTUME PAULO KUELEKEA WAYAHUDI WALIOISHI NJE YA PALESTINA
KABLA YA MKUTANO HUKO YERUSALEMU MWAKA WA 49 W.K.
Matendo 9:19, 20 Damasko — ‘akaanza kuhubiri katika masinagogi’
Matendo 9:29 Yerusalemu — “akiongea . . . na Wayahudi wenye kusema Kigiriki”
Matendo 13:5 Salami, Kipro — “kulitangaza neno la Mungu katika masinagogi ya Wayahudi”
Matendo 13:14 Antiokia huko Pisidia — “wakaingia ndani ya sinagogi”
Matendo 14:1 Ikoniamu — “wakaingia . . . katika sinagogi la Wayahudi”
BAADA YA MKUTANO HUKO YERUSALEMU MWAKA WA 49 W.K.
Matendo 16:14 Filipi — “Lidia, . . . mwabudu wa Mungu”
Matendo 17:1 Thesalonike — “sinagogi la Wayahudi”
Matendo 17:10 Beroya — “sinagogi la Wayahudi”
Matendo 17:17 Athene — “kujadiliana katika sinagogi pamoja na Wayahudi”
Matendo 18:4 Korintho — “akitoa hotuba katika sinagogi”
Matendo 18:19 Efeso — “akaingia ndani ya sinagogi akajadiliana na Wayahudi”
Matendo 19:8 Efeso — “akaingia katika sinagogi, akasema kwa ujasiri kwa miezi mitatu”
Matendo 28:17 Roma — “akawaita pamoja . . . wakuu wa Wayahudi”
-
-
Ukristo Waenea Miongoni mwa Wayahudi wa Karne Ya KwanzaMnara wa Mlinzi—2005 | Oktoba 15
-
-
Safari za Paulo na Wayahudi Walioishi Nje ya Palestina
Mgawo wa kwanza wa mtume Paulo ulikuwa “kupeleka jina [la Yesu Kristo] kwa mataifa na vilevile kwa wafalme na wana wa Israeli.”b (Matendo 9:15) Baada ya mkutano huo wa Yerusalemu, Paulo aliendelea kuwatembelea Wayahudi walioishi nje ya Palestina popote pale aliposafiri. (Ona sanduku kwenye ukurasa wa 14.) Yaelekea makubaliano hayo yalihusu maeneo wala si Wayahudi au watu wasio Wayahudi. Paulo na Barnaba walipanua kazi yao ya umishonari hadi upande wa magharibi, na wengine wakatumikia katika eneo la nyumbani la Wayahudi na katika jamii kubwa za Wayahudi zilizokuwa upande wa Mashariki.
Paulo na wenzake walipoanza safari yao ya pili ya umishonari kutoka Antiokia huko Siria, walielekea upande wa magharibi kupitia Asia Ndogo hadi Troa. Kutoka huko walivuka hadi Makedonia kwa sababu walikata kauli kwamba ‘Mungu alikuwa amewaita watangaze habari njema kwa Wamakedonia.’ Baadaye, makutaniko ya Kikristo yalianzishwa katika majiji mengine ya Ulaya, kutia ndani Athene na Korintho.—Matendo 15:40, 41; 16:6-10; 17:1–18:18.
Mwishoni mwa safari yake ya tatu ya umishonari, yapata mwaka wa 56 W.K., Paulo alipanga kusafiri mbali zaidi upande wa magharibi na kuhubiri zaidi katika eneo alilogawiwa kwenye mkutano wa Yerusalemu. Aliandika hivi: “Nina hamu ya kuitangaza habari njema kwenu pia mlio huko Roma,” na, “nitaondoka nikipitia kwenu kwenda Uhispania.” (Waroma 1:15; 15:24, 28)
-