-
Wokovu na Kushangilia Chini ya Utawala wa MesiyaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
13. (a) Isaya atoa wazo gani lenye kuchangamsha moyo? (b) Twajuaje kwamba amani anayoifafanua Isaya yahusisha mambo mengi kuliko tu usalama kutokana na wanyama wa mwituni?
13 Sasa Isaya atoa wazo lenye kusisimua moyo kuhusu hali ambazo Mungu ataleta nchini humo. Asema: “Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe. Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira. Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua BWANA [“Yehova,” “NW”], kama vile maji yanavyoifunika bahari.” (Isaya 11:6-9) Je, maneno hayo hayachangamshi moyo? Ona kwamba amani inayofafanuliwa hapo hutokana na kumjua Yehova. Basi, yanayohusika ni mengi kuliko tu usalama kutokana na wanyama wa mwituni. Kumjua Yehova hakutabadili wanyama, bali kutabadili watu. Waisraeli hawatahitaji kuogopa wanyama wa mwituni wala wanadamu walio kama wanyama wakiwa safarini wala wakiwa katika nchi yao iliyorudishwa.—Ezra 8:21, 22; Isaya 35:8-10; 65:25.
-
-
Wokovu na Kushangilia Chini ya Utawala wa MesiyaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
15. Je, twaweza kutarajia ifaavyo maneno ya Isaya yatimizwe kihalisi katika ulimwengu mpya? Eleza.
15 Je, unabii wa Isaya utakuwa na utimizo zaidi, labda ulio halisi zaidi, katika Paradiso itakayorudishwa? Yaonekana inafaa kufikiri hivyo. Unabii huo huwapa wote watakaoishi chini ya utawala wa Mesiya uhakikishio uleule uliowapa Waisraeli waliokuwa wakirudi; wao pamoja na watoto wao hawataogopa madhara kutoka popote—kwa binadamu au kwa wanyama. Chini ya utawala wa Ufalme wa Mesiya, wakazi wote wa dunia watafurahia hali zenye amani kama zile ambazo Adamu na Hawa walifurahia huko Edeni. Ni wazi kwamba Maandiko hayafunui mambo yote kuhusu namna maisha yalivyokuwa katika Edeni—wala vile yatakavyokuwa katika Paradiso. Hata hivyo, twaweza kuwa na uhakika kwamba, chini ya utawala wenye hekima na upendo wa Mfalme Yesu Kristo, kila jambo litakuwa kama istahilivyo.
-