Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sehemu ya 3—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Jambo la maana katika ujasiri na ustahimilivu wa Mashahidi lilikuwa kujengwa kwao na chakula cha kiroho. Ingawa ugavi wa fasihi ya kugawiwa wengine hatimaye ilipata kupungua sana katika sehemu nyingine za Ulaya wakati wa vita, walifaulu kueneza miongoni mwao habari yenye kujenga imani iliyokuwa imetayarishwa na Sosaiti kwa ajili ya funzo la Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote. Kwa kuhatirisha maisha zao, August Kraft, Peter Gölles, Ludwig Cyranek, Therese Schreiber, na wengine wengi walishiriki kazi ya kurudufisha na kugawanya habari ya funzo iliyoingizwa katika Austria kisirisiri kutoka Chekoslovakia, Italia, na Uswisi. Katika Uholanzi, ni mlinzi wa gereza mwenye fadhili aliyesaidia kwa kupata Biblia kwa ajili ya Arthur Winkler. Ijapokuwa tahadhari yote iliyochukuliwa na maadui, maji ya kweli ya Biblia yenye kuburudisha kutoka kwa Mnara wa Mlinzi yalifika hata ndani ya kambi za mateso za Ujerumani na kuenezwa miongoni mwa Mashahidi humo.

  • Sehemu ya 3—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Picha katika ukurasa wa 450]

      Wengine katika Austria na Ujerumani waliohatirisha maisha zao kwa kurudufisha au kugawanya habari yenye thamani ya funzo la Biblia, kama ile iliyoonyeshwa katika mandhari ya nyuma

      Therese Schreiber

      Peter Gölles

      Elfriede Löhr

      Albert Wandres

      August Kraft

      Ilse Unterdörfer

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki