Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Elimu ya Vitu vya Kale Inaunga Mkono Biblia?
    Amkeni!—2007 | Novemba
    • Unabii wa Isaya na Maandishi ya Koreshi

      Maandishi ya kale yaliyo katika bamba la udongo lililoonyeshwa hapa yanaunga mkono simulizi lingine la Biblia. Maandishi hayo yanayoitwa Cyrus Cylinder [9], yalipatikana katika eneo la Sipari ya kale kwenye Mto Efrati, kilomita 32 kutoka Baghdad. Yanataja jinsi Koreshi Mkuu, mwanzilishi wa Milki ya Uajemi, alivyoshinda Babiloni. Kwa kupendeza, miaka 200 hivi mapema, Yehova alikuwa amesema hivi kupitia nabii Isaya kuhusu mtawala wa Umedi na Uajemi ambaye angeitwa Koreshi: “‘Yeye ni mchungaji wangu, naye atatenda kikamilifu mapendezi yangu yote’; neno langu kuhusu Yerusalemu, ‘Atajengwa upya.’”—Isaya 13:1, 17-19; 44:26–45:3.

      Jambo lenye kutokeza ni kwamba maandishi hayo yanataja sera ya Koreshi, iliyotofautiana na ile ya washindi wengi wa kale. Koreshi aliwaruhusu watu waliokuwa wametekwa na utawala uliomtangulia warudi kwao. Historia inayopatikana katika Biblia na kutoka katika vyanzo vingine inathibitisha kwamba Koreshi aliwaruhusu Wayahudi warudi kwao, nao wakajenga upya Yerusalemu.—2 Mambo ya Nyakati 36:23; Ezra 1:1-4.

  • Je, Elimu ya Vitu vya Kale Inaunga Mkono Biblia?
    Amkeni!—2007 | Novemba
    • [Picha katika ukurasa wa 18 zimeandaliwa na]

      Photograph taken by courtesy of the British Museum

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki