-
Maji ya Uhai Yatiririka Katika Milima ya AndesMnara wa Mlinzi—2001 | Oktoba 15
-
-
Ziwa Titicaca lililo katika bonde la Milima ya Andes yenye kimo cha meta 3,800 juu ya usawa wa bahari, ndilo ziwa pekee barani linalotumiwa na vyombo vikubwa vya majini. Vilele vya milima vilivyofunikwa kwa theluji, ambavyo baadhi yavyo vina kimo cha meta zaidi ya 6,400, ni chemchemi ya karibu mito yote 25 inayoishia Titicaca. Kwa sababu sehemu hiyo imeinuka sana, tabia ya nchi ni baridi, na watu ambao si wenyeji, hupambana na magonjwa yanayopatikana katika nyanda za juu.
-
-
Maji ya Uhai Yatiririka Katika Milima ya AndesMnara wa Mlinzi—2001 | Oktoba 15
-
-
Mbali na visiwa hivi viwili vikubwa zaidi, habari njema pia zimehubiriwa katika visiwa vipatavyo 40 “vinavyoelea” kwenye Ziwa Titicaca. Visiwa vinavyoelea? Naam, visiwa hivi vimefanyizwa kwa totora, aina ya nyasi kubwa zinazokua katika sehemu fulani zisizo na kina za ziwa hilo. Nyasi hizo hukua na kuchomoza juu ya maji. Ili kujenga kisiwa, wenyeji hukunja nyasi hizo, zikiwa bado na mizizi, na kuzisokota ili kutengeneza jukwaa. Kisha jukwaa hilo hujazwa matope na kuimarishwa kwa kuongezewa nyasi zaidi. Watu huishi katika vibanda vilivyojengwa kwa nyasi juu ya jukwaa hizo.
-