-
Kukua Pamoja Katika UpendoMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Katika 1970, wakati Peru ilipopigwa na tetemeko la dunia lililo baya zaidi katika historia yayo, fedha za kitulizo cha dharura zilipelekwa haraka kutoka makao makuu ya ulimwengu katika New York, na tani 15 za nguo zikafuata. Hata hivyo kabla ya shehena hiyo kufika, Mashahidi walikuwa wameendesha msafara wa magari yakiwa na ugavi wa vitulizo katika maeneo ambayo majiji na vijiji vilikuwa vimeharibiwa, wakifanya hivyo katika muda wa saa chache baada ya barabara kufunguliwa. Kwa kuendelea katika siku na majuma yaliyofuata, waliandalia vikundi mbalimbali vilivyo juu katika milima Andes msaada uliohitajiwa kimwili na kiroho.
-
-
Kukua Pamoja Katika UpendoMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Picha katika ukurasa wa 311]
Mashahidi waliookoka tetemeko la dunia katika Peru walijenga jiji lao wenyewe la kimbilio na wakasaidiana
Ugavi wa vitulizo ulioletwa na Mashahidi wengine (chini) ulikuwa miongoni mwa ule wa kwanza kufika katika eneo hilo
-