Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uvuvi Katika Bahari ya Galilaya
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Oktoba 1
    • Wavuvi Wanaotajwa Katika Injili

      Vitabu vya Injili vinaonyesha wazi kwamba Simoni Petro alishirikiana na wengine katika biashara ya uvuvi. Watu hao alioshirikiana nao ndio waliokuja kumsaidia kuvuta wavu uliojaa samaki kimuujiza. (Luka 5:3-7) Wasomi fulani wanasema kwamba “wavuvi wangeweza kuunda ‘vyama vya ushirika’ . . . ili wakodi maeneo na wapate mikataba ya kuvua.” Huenda wana wa Zebedayo, Petro, Andrea, na washirika wao walifanya hivyo ili kupata idhini ya kuendesha biashara yao ya uvuvi.

      Maandiko hayatuambii waziwazi ikiwa wavuvi hao wa Galilaya walimiliki mashua na vifaa walivyotumia katika kazi yao. Watu fulani wanaamini kwamba walifanya hivyo. Kwa kweli inasemwa kwamba Yesu alipanda mashua “iliyokuwa ya Simoni.” (Luka 5:3) Hata hivyo, kitabu kimoja kilichozungumzia habari hiyo kinasema, “kuna uwezekano mkubwa mashua hizo zilikuwa za madalali na zilitumiwa na vyama vya wavuvi.”

  • Uvuvi Katika Bahari ya Galilaya
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Oktoba 1
    • a Ni wazi kwamba mtume Petro alihama kutoka Bethsaida hadi Kapernaumu ambako alifanya biashara ya uvuvi pamoja na ndugu yake, Andrea, na wana wa Zebedayo. Pia, Yesu aliishi huko Kapernaumu kwa muda fulani.—Mathayo 4:13-16.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki