-
Wahasmonia na Hali WaliyoachaMnara wa Mlinzi—2001 | Juni 15
-
-
Mafarisayo na Masadukayo wanatokea kama watu wenye ushawishi mkubwa, wenye uwezo wa kubadili maoni ya watu hata kufikia hatua ya kumkataa Yesu kuwa Mesiya. (Mathayo 15:1, 2; 16:1; Yohana 11:47, 48; 12:42, 43) Hata hivyo, makundi hayo mawili yenye ushawishi hayatajwi popote katika Maandiko ya Kiebrania.
Josephus anawataja Masadukayo na Mafarisayo mara ya kwanza katika karne ya pili K.W.K.
-
-
Wahasmonia na Hali WaliyoachaMnara wa Mlinzi—2001 | Juni 15
-
-
Anapoandika juu ya utawala wa Hyrcanus, ndipo Josephus kwanza anaandika juu ya uvutano unaozidi wa Mafarisayo na Masadukayo. (Josephus alikuwa ametaja Mafarisayo walioishi wakati wa utawala wa Jonathan.) Yeye hataji kama walikuwa na chanzo kimoja. Wasomi wengi wanaonelea kwamba walikuwa kikundi kilichotokana na Wasidim, madhehebu yenye kujitoa kwa Mungu iliyomwunga mkono Judah Maccabee katika kutimiza malengo yake ya kidini lakini wakamwacha wakati alipoanza kutamani mambo ya kisiasa.
-