Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Sayansi Imethibitisha Kwamba Hakuna Mungu?
    Amkeni!—2010 | Novemba
    • KWA miaka 50, mwanafalsafa Mwingereza Antony Flew, aliheshimiwa sana na wanasayansi wenzake kuwa mtetezi mkuu wa fundisho la kwamba hakuna Mungu. Kichapo chake “Theology and Falsification” (Theolojia na Uwongo) alichoandika mwaka wa 1950, “kilikuwa ndicho kichapo cha falsafa kilichochapishwa mara nyingi sana katika karne yote [ya 20].” Mnamo 1986, Flew aliitwa “mchambuzi mkuu wa fundisho la kwamba kuna Mungu.” Kwa hiyo, watu wengi walishtuka sana Flew alipotangaza katika mwaka wa 2004 kwamba amebadili maoni yake.

      Kwa nini Flew alibadili maoni yake? Kwa sababu ya sayansi. Alikuja kusadiki kwamba ulimwengu, sheria zinazoongoza vitu vya asili, na uhai haukujitokeza wenyewe tu.

  • Je, Sayansi Imethibitisha Kwamba Hakuna Mungu?
    Amkeni!—2010 | Novemba
    • Flew aliandika hivi katika mwaka wa 2007: “Jambo muhimu si kwamba tu kuna sheria za asili, bali ni kwamba sheria hizo ni sahihi kihisabati, ni za kweli kabisa, na ‘zina upatano.’ Einstein alisema kwamba ‘zinathibitisha kuwa kuna mtu mwenye akili aliyezibuni.’ Swali tunalopaswa kuuliza ni sheria hizi za asili zilitokea jinsi gani? Bila shaka hilo ndilo swali ambalo wanasayansi kuanzia wakati wa Newton kufikia wakati wa Einstein hadi wakati wa Heisenberg wameuliza—na wakajibu. Jibu lao ni zilitokezwa na Akili ya Mungu.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki