-
Kupiga Mbiu ya Kurudi kwa BwanaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Ilikuwa ile “Photo-Drama of Creation” (Drama-Picha ya Uumbaji)—muunganisho wa picha ya sinema na utoaji wa slaidipicha, ukiambatanishwa na muziki uliorekodiwa na hotuba zilizorekodiwa katika rekodi za santuri. Ilikuwa yenye urefu wa saa zapata nane na ilitolewa katika sehemu nne.
-
-
Kupiga Mbiu ya Kurudi kwa BwanaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Mbele ya wasikilizaji kulikuwapo kiwambo kikubwa cha kuonyeshea picha ya sinema. Walipokuwa wakitazama—na kusikiliza—jambo fulani lenye kustaajabisha kwelikweli likatukia. C. T. Russell, wakati huo akiwa katika miaka yake ya mapema ya 60, akatokea katika kiwambo. Midomo yake ikaanza kusema, na maneno yake yangeweza kusikika! Utoaji ulipoendelea, ulipeleka wahudhuriaji—kwa njia ya maneno, picha za rangi, na muziki—kutoka uumbaji wa dunia mpaka mwisho wa Utawala wa Miaka Elfu wa Kristo. Katika pindi ya utoaji waliona pia (kwa njia ya upigaji picha wa kuongeza mwendo) mambo mengine ambayo yalistaajabisha—kufunuka kwa ua na kuanguliwa kwa kifaranga. Walivutiwa kwelikweli!
-