Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tajiri Ingawa Maskini—Yawezekanaje?
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Septemba 15
    • Thamani ya Funzo la Biblia

      Mashahidi wa Yehova huthamini funzo la Neno la Mungu, Biblia, na walio maskini kati yao hawawi tofauti. John mwenye umri wa miaka 60 hutumika kutanikoni akiwa painia (mhubiri wa wakati wote wa Ufalme) na mtumishi wa huduma. Anaishi katika jengo lenye orofa mbili lililochakaa ambako familia 13 hukaa. Chumba chake ni sehemu ya ukumbi wa orofa ya kwanza, ambacho kimegawanywa kwa mbao. Ndani yake mna viti viwili vya zamani na meza ambayo juu yake vichapo vya kusaidia kujifunza Biblia vimerundamana. Yeye hulalia mkeka wa nyasi.

      John alikuwa akichuma dola moja kwa siku kwa kuuza mkate, lakini uingizaji wa ngano kutoka nje ulipopigwa marufuku, alipoteza njia hii ya kupata riziki. Yeye asema hivi: “Napata maisha kuwa magumu sana nyakati nyingine, lakini ninaendelea kupainia. Yehova ndiye hunitegemeza. Mimi hufanya kazi yoyote niwezayo kupata na sitegemei binadamu yeyote anitegemeze au kunilisha, ingawa ndugu kutanikoni ni wenye kusaidia sana. Wao hunisaidia kutafuta kazi na nyakati nyingine hunipa zawadi za fedha.

      “Mimi hutenga wakati wa kusoma Biblia na vichapo vya Watch Tower Society. Mimi hujifunza saa za alfajiri wakati ambapo nyumba ni kimya na husoma baadaye usiku wakati wowote tunapokuwa na stima. Najua lazima niendeleze funzo langu la kibinafsi.”

  • Tajiri Ingawa Maskini—Yawezekanaje?
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Septemba 15
    • Joan, anayeishi Afrika ya Kati, ni painia. Ili kutunza mumeye aliyepooza na watu wengine wanne wanaomtegemea, yeye huuza mikate. Kutaniko ambalo yeye huhudhuria lilipohitaji benchi kwa ajili ya Jumba la Ufalme, familia ya Joan iliamua kutoa fedha zote walizokuwa nazo nyumbani. Kufanya hivyo kuliwaacha bila fedha zozote. Hata hivyo, siku iliyofuata, mtu fulani aliwalipa deni la muda mrefu bila kutazamiwa, akiwapa fedha ambazo walikuwa hawana matumaini ya kuzipata kamwe!

      Joan ni mwenye uchangamfu na hana wasiwasi wa kupita kiasi juu ya fedha. “Mimi humweleza Yehova hali yangu katika sala, na kisha huenda kwenye huduma ya shambani. Twajua kwamba kuna matumaini kidogo ya hali bora zaidi katika huu mfumo wa mambo. Lakini, twang’amua kwamba Yehova atatuandalia mahitaji yetu.”

  • Tajiri Ingawa Maskini—Yawezekanaje?
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Septemba 15
    • Bila shaka, katika mahali pengi haiwezekani kabisa kupata kazi. Mzee Mkristo ambaye hutumikia kwenye mojawapo ya ofisi za tawi za Watch Tower Society katika Afrika ya Kati aliandika hivi: “Ndugu wengi hapa hawana kazi. Baadhi yao hujaribu kubuni kazi zao wenyewe, lakini jambo hilo ni gumu. Wengi wamesababu kwamba kwa kuwa watateseka hata wakifanya nini, watadhabihu faida za kimwili wakiwa wahudumu mapainia. Kwa kufanya hivyo, wengi hupata kwamba wanabarikiwa kwa wingi zaidi kuliko wakiwa na kazi ya mshahara kidogo au bila mshahara wowote.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki