Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na wao walipewa mamlaka juu ya sehemu ya nne ya dunia, kuua kwa upanga mrefu na kwa upungufu wa chakula na kwa tauni yenye kufisha na kwa hayawani-mwitu wa dunia.” (Ufunuo 6:8b, NW)

  • Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 28. (a) Kumekuwaje na utimizo wa unabii kuhusu “tauni yenye kufisha”? (b) Watu wa Yehova wamepewaje himaya juu ya magonjwa mengi leo?

      28 Lenye umaana wa kisasa hapa ni “tauni yenye kufisha.” Kufuata mikumbo ya Vita ya Ulimwengu 1, homa-mafua ya Hispania ilivuna maisha za binadamu milioni 20 katika miezi michache tu ya 1918-19. Eneo pekee duniani lililoepuka pigo hili ni kisiwa kidogo cha St. Helena. Katika mahali ambako idadi ya watu waliuawa sana na ugonjwa huu marundo ya kuni za maziko yaliwashwa ili kuchoma maiti chunguchungu. Na leo kuna tukio lenye kuogofya la ugonjwa wa moyo na kansa, na chenye kuyasababisha sana ni uchafuzi wa tumbako. Katika kile kilichoelezwa kuwa “mwongo wenye sura mbaya” wa miaka ya 1980, njia ya maisha ambayo ni ya uasi wa sheria kulingana na viwango vya Biblia iliongeza lile pigo la UKIMWI kwa ile “tauni yenye kufisha.” Katika mwaka wa 2,000, iliripotiwa kwamba daktari mkuu wa Marekani alisema kwamba “huenda [UKIMWI] ndio ugonjwa mbaya zaidi wenye kuambukiza uliopata kutokea ulimwenguni.” Alisema kwamba watu milioni 52 ulimwenguni pote walikuwa na virusi vya UKIMWI, na milioni 20 kati yao tayari walikuwa wamekufa. Jinsi watu wa Yehova walivyo wenye shukrani kwamba lile shauri la hekima la Neno lake linawaepusha na uasherati na tumizi baya la damu, ambalo kupitia kwalo magonjwa mengi sana yanapitishwa leo!—Matendo 15:28, 29, NW; linga 1 Wakorintho 6:9-11.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki