-
Hobi Yangu Ni AstronomiaAmkeni!—1996 | Agosti 8
-
-
Nyota au Sayari?
Kuona sehemu nyangavu zaidi ya nuru huzusha swali, Je, ni nyota au ni sayari? Nyota ni vyanzo vya nuru, injini kuu za kinyuklia zinazotokeza viishara vya sumakuumeme angani. Ziko mbali sana na dunia, ya karibu zaidi—kando na jua—ikiwa umbali wa miaka-nuru 4.3. Nuru husafiri kwa kilometa 299,000 hivi kwa sekunde. Kwa kuwa nuru kutoka katika nyota husafiri mbali sana ili kutufikia, hiyo huwa hafifu. Kisha ni lazima ipitie unene wa angahewa la dunia, ambao hupinda-pinda miale ya nuru. “Metameta, nyota ndogo, jinsi nishangaavyo kile ulicho,” wasema wimbo wa nasari, ukiongeza uhai katika mbingu zenye ukimya. Ikimetameta, hiyo ni nyota.
Hata hivyo, sayari, huakisi tu nuru kutoka kwa jua, kama tu vile mwezi ufanyavyo. Hizo ziko karibu zaidi nasi, zikiwa washiriki wa familia ya jua, mfumo wa jua. Kwa hiyo sayari ziwezazo kuonwa kwa macho matupu huakisi nuru ambayo ni thabiti na isiyometameta.
-
-
Hobi Yangu Ni AstronomiaAmkeni!—1996 | Agosti 8
-
-
Kujua kwamba unatazama sayari kunathibitishwa na kutazama kwa siku zenye kufuatana, kwa sababu sayari haikai mahali pamoja tofauti na nyota zisizosonga.
-