Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maandishi Yaliyopotea ya John Milton
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Septemba 15
    • NI VIGUMU kumpata mwandishi ambaye alikuwa na uvutano mkubwa sana katika ulimwengu kama John Milton, mtungaji wa shairi maarufu la Kiingereza linaloitwa Paradiso Iliyopotezwa (Paradise Lost).

  • Maandishi Yaliyopotea ya John Milton
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Septemba 15
    • Leo, John Milton anajulikana sana kwa sababu ya kutunga shairi linaloitwa Paradiso Iliyopotezwa ambalo linasimulia habari ya Biblia kuhusu jinsi mwanadamu alivyopoteza ukamilifu. (Mwanzo, sura ya 3) Shairi hilo hasa ambalo lilichapishwa mwaka wa 1667, ndilo lililomfanya Milton awe mwandishi mashuhuri, hasa katika nchi zilizozungumza Kiingereza. Baadaye, alichapisha shairi la pili lenye kichwa Paradiso Iliyorudishwa (Paradise Regained). Mashairi hayo yanaonyesha kusudi la kwanza la Mungu kwa ajili ya mwanadamu, yaani, kufurahia uhai mkamilifu katika paradiso duniani, na yanataja jinsi Mungu atakavyorudisha Paradiso duniani kupitia Kristo. Kwa mfano, katika shairi la Paradiso Iliyopotezwa, Mikaeli yule malaika mkuu anatabiri wakati ambapo Kristo “atawathawabisha waaminifu Wake, na kuwapa furaha ya milele, iwe mbinguni au duniani, kwa kuwa wakati huo dunia yote itakuwa paradiso, na itakuwa na furaha zaidi kuliko furaha ya Edeni, na maisha yatakuwa yenye furaha zaidi.”

  • Maandishi Yaliyopotea ya John Milton
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Septemba 15
    • [Picha katika ukurasa wa 12]

      Shairi “Paradiso Iliyopotezwa” lilimfanya Milton awe mtu maarufu

      [Hisani]

      Courtesy of The Early Modern Web at Oxford

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki