-
Walijaribu Kuwazuia Watu Wasilipate Neno la MunguAmkeni!—2011 | Desemba
-
-
Mnamo 1199, Papa Innocent wa Tatu aliandika kuhusu watu walioonwa kuwa wazushi ambao walitafsiri Biblia katika Kifaransa na wakaamua kuwa na mazungumzo kati yao kuihusu. Innocent alitumia maneno haya ya Yesu kuwahusu: “Msiwape mbwa kitu kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe.” (Mathayo 7:6) Kwa nini alikuwa na maoni hayo? “Ili mtu wa kawaida na ambaye hana elimu asiwe na kimbelembele cha kujifunza Maandiko matakatifu yaliyotukuka, au kuwahubiria watu kuyahusu.” Mara nyingi, wale waliopinga amri ya papa walipelekwa kwa watesaji ambao waliwalazimisha waungame kwamba wao ni wazushi. Wale waliokataa kukana msimamo wao waliteketezwa wakiwa hai.
Wakati wa kile kipindi kirefu cha kuwazuia watu wasiipate na kuisoma Biblia, barua ya Papa Innocent ilitumiwa mara nyingi ili kutetea wazo la kwamba Biblia haipaswi kutumiwa wala kutafsiriwa katika lugha nyingine. Punde tu baada ya amri yake kutolewa, Biblia katika lugha nyingine zikaanza kuteketezwa, na pia watu fulani waliomiliki Biblia waliteketezwa. Katika karne zilizofuata, maaskofu na watawala wa nchi za Ulaya zilizokuwa chini ya udhibiti wa Kanisa Katoliki walitumia njia yoyote waliyoweza ili kuhakikisha kwamba marufuku yaliyowekwa na Papa Innocent wa Tatu yalifuatwa.
-
-
Walijaribu Kuwazuia Watu Wasilipate Neno la MunguAmkeni!—2011 | Desemba
-
-
1199
Papa Innocent wa Tatu anasema kwamba wote wanaojaribu kutafsiri au kuwa na mazungumzo kuhusu Biblia ni wazushi. Wale wanaopinga amri ya papa wanateswa na kuuawa
-