-
Makanisa YaungamaMnara wa Mlinzi—1998 | Machi 1
-
-
Papa Aombapo Msamaha
Kati ya mwaka wa 1980 na 1996, John Paul wa Pili ‘alitambua makosa ya kihistoria ya Kanisa au akaomba msamaha’ angalau mara 94, asema mwelezaji wa Vatikani Luigi Accattoli katika kitabu chake Quando il papa chiede perdono (Papa Aombapo Msamaha). Kulingana na Accattoli, “katika Kanisa Katoliki, ni papa tu awezaye kufanya ungamo.” Naye amefanya hilo, akirejezea matukio yenye kubishaniwa zaidi katika historia ya Katoliki—zile Krusedi, vita, kutegemeza udikteta mbalimbali, migawanyiko katika kanisa, uhasama kuelekea watu wa Kiyahudi, yale Mabaraza ya Kuhukumu Wazushi, Mafia, na ubaguzi wa kijamii. Katika taarifa iliyopelekewa makadinali mwaka wa 1994 (ambayo yaonwa na wengine kuwa hati ya maana zaidi ya ofisi ya papa), John Paul wa Pili alipendekeza “ungamo la dhambi la ujumla na la milenia.”
-
-
Kwa Nini Yanaomba Msamaha?Mnara wa Mlinzi—1998 | Machi 1
-
-
Mwanahistoria Mkatoliki Nicolino Sarale alitaarifu kwamba katika “mradi [wa John Paul wa Pili] wa ‘maungamo,’ kuna mkakati, nao ni muungano wa kidini.”
Hata hivyo, mengi zaidi ya muungano wa kidini yahusishwa. Leo, historia yenye sifa mbaya ya Jumuiya ya Wakristo yajulikana sana. “Ukatoliki hauwezi kuipuuza tu historia yote hiyo,” asema mwanatheolojia Hans Urs von Balthasar. “Kanisa lake mwenyewe limefanya au limeruhusu kufanywa kwa mambo ambayo bila shaka hatuwezi kuyakubali siku hizi.” Kwa sababu hiyo, papa ameweka tume ya “kueleza rekodi mbovu ya kanisa ili . . . msamaha uweze kuombwa.” Basi, sababu nyingine ya kanisa kunuia kushiriki katika kujichambua yaonekana kuwa tamaa ya kupata tena msimamo wake wa kiadili.
-
-
Kwa Nini Yanaomba Msamaha?Mnara wa Mlinzi—1998 | Machi 1
-
-
Si wote wakubalio kwamba makanisa yapaswa kuomba msamaha waziwazi. Kwa kielelezo, idadi fulani ya washiriki wa Katoliki ya Kiroma huhisi kutostarehe wakati ambapo papa wao huomba msamaha kwa sababu ya utumwa au awarudishiapo sifa njema “wazushi” kama vile Hus na Calvin. Kulingana na vyanzo vya Vatikani, hati iliyopelekwa kwa makadinali ikipendekeza “uchunguzi wa dhamiri” katika historia ya Ukatoliki ya mileani iliyopita ilichambuliwa na makadinali waliokuwa wakihudhuria baraza la papa na makadinali lililofanywa Juni 1994. Hata hivyo papa alipotaka kutia ndani sehemu ya msingi ya pendekezo hilo katika waraka wa papa, kadinali Mwitalia Giacomo Biffi alitoa taarifa ya pasta ambamo alithibitisha: “Kanisa halina dhambi yoyote.” Hata hivyo, alikubali hivi: “Kuomba msamaha kwa sababu ya makosa ya kanisa ya karne zilizopita . . . kwaweza kutumika kutufanya tuwe wenye kukubalika zaidi.”
“Kuungama dhambi ni mojawapo ya habari yenye kubishaniwa zaidi katika Kanisa Katoliki,” asema mwelezaji wa Vatikani Luigi Accattoli. “Papa akikiri makosa ya wamishonari, kuna wamishonari ambao hupinga hilo kwa nia njema.” Zaidi, mwandishi wa habari wa Katoliki ya Kiroma aliandika hivi: “Ikiwa kwa kweli papa ana wazo lenye kuhofisha hivyo juu ya historia ya Kanisa, ni vigumu kuelewa jinsi yeye awezavyo kulionyesha Kanisa lilo hilo kuwa mhusika mkuu mwenye kutokeza wa ‘haki za kibinadamu,’ ‘mama na mwalimu’ ambaye yeye peke yake aweza kuongoza jamii ya binadamu kuingia katika mileani ya tatu yenye matumaini mema kwelikweli.”
-
-
Kwa Nini Yanaomba Msamaha?Mnara wa Mlinzi—1998 | Machi 1
-
-
Katika kusema juu ya maungamo ya papa ya kurudia-rudia, Kadinali Biffi aliuliza hivi kwa kukejeli: “Kwa ajili ya dhambi za kihistoria, je, haingekuwa afadhali kwetu sote kungojea hukumu ya ulimwengu wote mzima?” Hukumu ya wanadamu wote inakaribia. Yehova Mungu ajua vema matukio yote maovu katika historia ya dini. Upesi vya kutosha, atawatoza hesabu wenye hatia. (Ufunuo 18:4-8)
-