Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Idadi ya Watu, Biblia, na Wakati Ujao
    Amkeni!—2004 | Mei 8
    • Ongezeko la Idadi ya Watu Baada ya Gharika

      Biblia inasema kwamba ni watu wanane tu waliookoka Gharika ya siku za Noa. Wataalamu fulani wa takwimu wanakadiria kwamba miaka 1,400 hivi baadaye, huenda idadi ya watu ulimwenguni ilifikia milioni 50. Je, inawezekana watu kuongezeka kutoka watu 8 hadi milioni 50 katika miaka 1,400?

      Kwanza kabisa, idadi ya watu milioni 50 ni kadirio tu. Hata hivyo, inafaa kuona vile Biblia inavyosema kwenye Mwanzo 9:1: “Naye Mungu akambariki Noa na wanawe, akawaambia: ‘Zaeni, muwe wengi, mjaze dunia.’” Kisha, katika sura ya 10 na 11, tunasoma juu ya familia 70 ambazo zilitokana na wana wa Noa—Shemu, Hamu, na Yafethi. Tunapoendelea kusoma, tunafikia ukoo wa Shemu hadi Abrahamu, ambao ‘walizaa wana na mabinti.’ Huenda wakati huo watu walizaa sana kulingana na amri ya Mungu ya ‘kuijaza dunia.’

      Namna gani idadi ya watu waliokufa? Sura hizo za Mwanzo zinaeleza pia jinsi wanadamu walivyoishi maisha marefu sana miaka mingi baada ya Gharika.a Wakati watu wanapozaliwa sana na wachache kufa, kunakuwa na ongezeko la haraka.

  • Idadi ya Watu, Biblia, na Wakati Ujao
    Amkeni!—2004 | Mei 8
    • a Baadaye, maisha ya wanadamu yalipungua hadi miaka 70 au 80 kama ilivyoonyeshwa na Musa karibu mwaka wa 1500 K.W.K.—Zaburi 90:10.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki