Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maskini Wanazidi Kuwa Maskini
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Agosti 1
    • Tofauti kati ya matajiri na maskini inaonekana wazi zaidi. Huko Ufilipino, theluthi moja ya watu hujitegemeza kwa kiasi kinachopungua dola moja ya Marekani kwa siku, kiasi ambacho mara nyingi huchumwa kwa dakika chache katika mataifa tajiri. Kichapo cha Umoja wa Mataifa, Human Development Report 2002 kinasema kwamba “mapato ya asilimia 5 ya watu matajiri sana ulimwenguni ni mara 114 zaidi ya asilimia 5 ya wale walio maskini sana.”

  • Maskini Wanazidi Kuwa Maskini
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Agosti 1
    • Likinukuu ripoti ya Shirika la Marekani la Sensa ya 2001, gazeti The New York Times lilionyesha kwamba pengo kati ya matajiri na maskini huko Marekani linazidi kupanuka. Lilisema hivi: “Asilimia 20 ya watu walio matajiri sana ilipokea nusu ya mapato ya familia zote mwaka jana . . . Asilimia 20 ya walio maskini sana ilipokea asilimia 3.5.” Hali iko hivyo au ni mbaya hata zaidi katika nchi nyingine nyingi. Ripoti moja ya Benki ya Dunia inaonyesha kwamba asilimia 57 ya watu ulimwenguni hujitegemeza kwa kiasi kinachopungua dola mbili kwa siku.

      Kufanya hali iwe mbaya hata zaidi, katika mwaka wa 2002, watu wengi walikerwa na ripoti kuhusu wasimamizi wa makampuni ambao walitajirika kwa njia zenye kutiliwa shaka. Hata kama utajiri huo ulipatikana kwa njia halali, wengi wamehisi kwamba wasimamizi hao wa makampuni “walikuwa matajiri kupita kiasi, bila kujali wengine,” kama lilivyosema gazeti Fortune. Kwa kufikiria yale yanayotukia ulimwenguni, wengine hujiuliza kama kweli ni haki kwa watu fulani kuwa na pesa nyingi mno, ambazo zinakadiriwa kuwa mamilioni ya dola, huku wengine wakiishi katika umaskini.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki