Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uwe na Bidii kwa Ajili ya Nyumba ya Yehova!
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Juni 15
    • 9. Ni tishio gani ambalo Yehoshafati na Yuda walikabili, na walitenda jinsi gani?

      9 Yehoshafati alitawala akiwa mfalme huko Yuda katika karne ya kumi K.W.K. Yeye na wakaaji wote wa Yuda walikabili tishio la majeshi ya muungano ya Waamoni, Wamoabu, na watu wa eneo lenye milima la Seiri. Ingawa aliogopa, mfalme huyo alifanya nini? Yeye na watu wake, wakiwa pamoja na wake na watoto wao, walikusanyika kwenye nyumba ya Yehova ili kusali. (Soma 2 Mambo ya Nyakati 20:3-6.) Kupatana na maneno ambayo Sulemani alisema mapema wakati wa kuliweka wakfu hekalu, Yehoshafati alitoa dua akisema: “Ee Mungu wetu, je, hutafanya hukumu juu yao? Kwa maana hakuna nguvu ndani yetu mbele ya umati huu mkubwa unaokuja juu yetu; nasi wenyewe hatujui tunalopaswa kufanya, lakini macho yetu yanakuelekea wewe.” (2 Nya. 20:12, 13)

  • Uwe na Bidii kwa Ajili ya Nyumba ya Yehova!
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Juni 15
    • Ikiwa nyakati fulani tunajikuta katika hali ngumu, tusijue jambo la kufanya, acheni tufuate mfano mzuri wa Yehoshafati na watu wa Yuda na kusali kwa Yehova huku tukimtegemea kabisa. (Met. 3:5, 6; Flp. 4:6, 7) Hata ikiwa tunaishi mbali na waamini wenzetu, maombi yetu kwa Yehova yanatuunganisha na “ushirika mzima wa ndugu [zetu] ulimwenguni.”—1 Pet. 5:9.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki