Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutumikia Kwa Shangwe Licha ya Magonjwa
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Juni 1
    • Wakati huo mgumu zaidi maishani mwangu, nilisali sana kwa Yehova kuliko wakati mwingine wowote, na kumweleza kwa unyoofu wasiwasi na mahangaiko yangu yote. Nilisali usiku na mchana nikitokwa machozi. Baada ya muda nilifarijika. Niliona maneno haya yenye kufariji ya Wafilipi 4:6, 7 yakitimia katika kisa changu: “Msihangaike juu ya kitu chochote, bali katika kila jambo kwa sala na dua pamoja na kutoa shukrani maombi yenu na yajulishwe Mungu; na amani ya Mungu yenye ubora unaozidi fikira zote itailinda mioyo yenu na nguvu zenu za akili kwa njia ya Kristo Yesu.”

  • Kutumikia Kwa Shangwe Licha ya Magonjwa
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Juni 1
    • Sala ni msaada mwingine mkubwa kutoka kwa Yehova wa kuwaimarisha watumishi wake. (Zaburi 65:2) Yehova amejibu sala zangu kwa kunipa nguvu za kuendelea katika imani kwa miaka yote hiyo. Hasa ninapohisi nimevunjika moyo, sala hunituliza na kunisaidia kudumisha shangwe. Kuwasiliana na Yehova kwa ukawaida hunichangamsha na kunichochea kuendelea kusonga mbele. Ninasadiki kabisa kwamba Yehova husikia sala za watumishi wake na kuwapa amani ya akili wanayohitaji.—Zaburi 51:17; 1 Petro 5:7.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki