-
Kupiga Mbiu ya Kurudi kwa BwanaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Kwa miongo ya miaka Russell na washirika wake walikuwa wamekuwa wakipiga mbiu kwamba Nyakati za Mataifa zingekoma katika 1914. Matarajio yalikuwa makubwa. C. T. Russell alikuwa amechambua wale waliokuwa wameweka tarehe mbalimbali za kurudi kwa Bwana, kama vile William Miller na baadhi ya vikundi vya Waadventisti wa Pili. Hata hivyo, tangu wakati wa ushirika wake wa mapema na Nelson Barbour, yeye alisadiki kwamba kulikuwa na kronolojia iliyokuwa sahihi, ikitegemea Biblia, na kwamba ilielekeza kwenye mwaka 1914 kuwa mwisho wa Nyakati za Mataifa.
-
-
Kupiga Mbiu ya Kurudi kwa BwanaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 60]
“Jihadharini na 1914!”
Wakati Vita ya Ulimwengu 1 ilipofyatuka katika 1914, “The World,” wakati huo likiwa gazeti kuu la habari katika New York City, lilitaarifu hivi katika sehemu ya jarida: “Ule mfyatuko wa vita wenye kuogofya katika Ulaya umetimiza unabii wenye kutokeza. . . . ‘Jihadharini na 1914!’ ndicho kimekuwa kilio cha mamia ya waevanjeli wasafirio, ambao, wakiwakilisha imani hii ya kigeni [iliyoshirikishwa na Russell], wameenda huku na huku nchini wakieleza fundisho kwamba ‘Ufalme wa Mungu umekaribia.’”—“The World Magazine,” Agosti 30, 1914.
-