Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mikusanyiko Uthibitisho wa Udugu Wetu
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Katika Kitwe, Rhodesia Kaskazini (sasa Zambia), katika kitovu cha Kanda ya Shaba, mkusanyiko uliratibiwa ufanywe wakati wa ziara ya msimamizi wa Watch Tower Society katika 1952. Mahali palikuwa eneo kubwa katika viunga vya mojawapo kambi za kuchimba shaba, katika mahali pajulikanapo sasa kuwa Chamboli. Sehemu ya juu ya kichuguu ilisawazishwa, na paa ikajengwa juu yayo itumike kuwa jukwaa. Vibanda vingine vilijengwa kwa ajili ya mahali pa kulala, pamoja na vitanda, kimoja juu ya kingine, zikitokeza meta 180 kutoka eneo kuu la kuketi kama njukuti (spoku) katika gurudumu la baiskeli. Wanaume na wavulana walilala katika baadhi yavyo; na wanawake na wasichana katika vile vingine. Baadhi ya wajumbe walikuwa wamesafiri kwa baiskeli kwa majuma mawili ili wawepo. Wengine walikuwa wametembea kwa siku kadhaa na kisha wakamaliza safari kwa kupanda basi la kikale.

      Wakati wa vipindi wale waliokuwa miongoni mwa wasikilizaji walisikiliza kwa hamu sana, ingawa waliketia mabenchi magumu ya mianzi katika mahali palipo wazi. Walikuwa wamekuja kusikia, nao hawakutaka kukosa neno hata moja. Uimbaji wa idadi hiyo ya wasikilizaji 20,000 na kutoa machozi machoni—ulikuwa mzuri sana. Hakukuwa na ufuatishaji wa vyombo vya muziki, lakini upatano wa sauti ulikuwa mzuri sana. Si katika kuimba kwao tu bali katika kila njia, umoja ulidhihirika miongoni mwa Mashahidi hawa, ingawa walitoka katika malezi ya namna nyingi na makabila mengi.

  • Mikusanyiko Uthibitisho wa Udugu Wetu
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Picha katika ukurasa wa 269]

      Mkusanyiko wa mahali palipo wazi katika Kitwe, Rhodesia Kaskazini, wakati wa ziara ya N. H. Knorr katika 1952

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki