Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sikiliza Shauri, Kubali Nidhamu
    Mwabudu Mungu wa Pekee wa Kweli
    • Mifano ya Kufikiria Tunaposhauriwa

      3, 4. (a) Biblia ina nini kinachoweza kutusaidia kuwa na maoni yanayofaa kuhusu shauri na nidhamu? (b) Mfalme Sauli aliitikiaje aliposhauriwa, na matokeo yalikuwa nini?

      3 Neno la Mungu linaeleza juu ya watu ambao walishauriwa walipokosea. Wengine walishauriwa kisha wakatiwa nidhamu. Mfano mmoja ni ule wa Mfalme Sauli wa Israeli aliyekataa kutii maagizo ya Yehova kuhusu taifa la Amaleki. Waamaleki walikuwa wamewapinga watumishi wa Mungu, na Yehova aliagiza kwamba Waamaleki wote waangamizwe pamoja na mifugo yao. Lakini Mfalme Sauli hakumwangamiza mfalme wao na mifugo yao bora.—1 Samweli 15:1-11.

      4 Yehova alimtuma nabii Samweli amkaripie Sauli. Sauli aliitikiaje? Alibisha kwamba aliwashinda Waamaleki lakini akaamua tu kumwacha mfalme wao. Lakini alikiuka amri ya Yehova kwa kufanya hivyo. (1 Samweli 15:20) Sauli alijaribu kuwalaumu watu kwa sababu ya kuiacha mifugo, alisema: “Naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao.” (1 Samweli 15:24) Yaonekana kwamba alihangaikia mno sifa yake, hata akamwomba Samweli amheshimu mbele ya watu. (1 Samweli 15:30) Mwishowe, Yehova alimkataa Sauli asiwe mfalme.—1 Samweli 16:1.

  • Sikiliza Shauri, Kubali Nidhamu
    Mwabudu Mungu wa Pekee wa Kweli
    • 6. (a) Kwa nini Sauli na Uzia walikataa shauri? (b) Kwa nini kukataa shauri ni tatizo zito leo?

      6 Kwa nini Sauli na Uzia walikataa shauri? Tatizo hasa lilikuwa kiburi, kila mmoja wao alijiona kuwa mtu wa maana sana. Watu wengi hujiletea msiba kwa sababu ya sifa hiyo. Wao hufikiri kwamba wataonekana kuwa dhaifu au sifa yao itaharibika wakikubali shauri. Lakini kiburi ni udhaifu. Kiburi humpumbaza mtu na kumfanya akatae msaada ambao Yehova anatoa kupitia Neno na tengenezo lake. Kwa hiyo, Yehova anaonya hivi: “Kiburi hutangulia uangamivu; na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.”—Mithali 16:18; Waroma 12:3.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki