Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 1
    • Mawe ya thamani kwenye kifuko cha kifuani cha kuhani mkuu wa Israeli yalitoka wapi?

      ▪ Baada ya Waisraeli kuondoka Misri na kuingia nyikani, Mungu aliwapa maagizo ya kutengeneza kifuko cha kifuani. (Kutoka 28:15-21) Kifuko hicho kilikuwa na mawe ya thamani kama vile, zibarijadi, topazi, zumaridi, feruzi, yakuti, yaspi, leshemi, akiki, amethisti, krisolito, shohamu, na yashefi.a Je, kweli Waisraeli wangepata mawe hayo mbalimbali yenye thamani?

      Katika nyakati za Biblia watu walithamini sana mawe yenye thamani na hata waliyatumia katika biashara. Kwa mfano, Wamisri wa kale walipata mawe yenye thamani kutoka maeneo ya mbali, kama vile nchi ambazo sasa ni Iran, Afghanistan, na huenda hata India. Migodi iliyokuwa Misri ilikuwa na aina mbalimbali za mawe yenye thamani. Wafalme wa Misri walimiliki uchimbaji wa madini katika maeneo waliyoyadhibiti. Mzee wa ukoo Ayubu alifafanua jinsi rafiki zake walivyotumia vifaa vya kuchimba ili kutafuta hazina. Kati ya mawe yenye thamani yaliyochimbwa ardhini, Ayubu anataja kihususa yakuti na topazi.​—Ayubu 28:1-11, 19.

      Simulizi kwenye kitabu cha Kutoka linasema kwamba Waisraeli walipoondoka ‘waliwaacha Wamisri bila chochote.’ (Kutoka 12:35, 36) Kwa hiyo, inawezekana kwamba Waisraeli walitoa Misri mawe yenye thamani waliyoweka kwenye kifuko cha kifuani cha kuhani mkuu.

  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 1
    • a Leo inaweza kuwa vigumu kutambua majina ya kisasa ya mawe hayo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki