Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kufahamu Kanuni Hudhihirisha Ukomavu
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Oktoba 15
    • MASHIRIKA mabaya huharibu mazoea yenye mafaa. Unavuna unachopanda. (1 Wakorintho 15:33; Wagalatia 6:7) Kila taarifa ni kielelezo cha kweli ya msingi—kanuni—ama kimwili ama kiroho, na kila moja huandaa msingi kwa ajili ya sheria. Ingawa hivyo, huenda sheria zikawa za muda tu, na huelekea kuwa mahususi. Kanuni, kwa upande ule mwingine, ni pana, na zaweza kudumu milele. Hivyo, Neno la Mungu hututia moyo tufikiri kupatana na kanuni popote iwezekanapo.

      Kichapo cha Webster’s Third New International Dictionary hufafanua kanuni kuwa “kweli ya ujumla au ya msingi: sheria, fundisho, au dhana iliyo pana na ya msingi ambayo juu yake nyingine hutegemezwa au kutolewa.” Kwa kielelezo, huenda mmoja akamtolea mtoto sheria, “Usiguse jiko kamwe.” Lakini kwa mtu mzima taarifa, “Jiko lina moto” ingetosha. Ona kwamba taarifa ya mwisho ni ya msingi zaidi. Kwa sababu yaongoza lile ambalo mmoja huenda akafanya—labda kupika, kuoka au kuzima jiko—kwa maana fulani inakuwa kanuni.

      Bila shaka, kanuni za msingi za maisha ni za kiroho; hizo huongoza kumwabudu kwetu Mungu na furaha yetu. Ingawa hivyo, watu fulani huacha kufanya jitihada zitakwazo ili kusababu juu ya kanuni. Wao hupendelea ule urahisi wa sheria wakabiliwapo na uamuzi. Hilo si jambo la hekima na hutofautiana na kielelezo kilichotolewa na watu wa zamani katika nyakati za Biblia.—Waroma 15:4.

  • Kufahamu Kanuni Hudhihirisha Ukomavu
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Oktoba 15
    • Chunguza Kanuni Itegemezayo Sheria

      Bila shaka, sheria hutekeleza fungu muhimu katika maisha ya Mkristo. Hizo ni kama walinzi ambao husaidia kutuhami, na kwenye msingi wa hizo sheria kuna kanuni nyingi za maana. Kukosa kufahamu kanuni hizo huenda kukapunguza kupenda kwetu sheria zenye kuhusiana na hizo kanuni. Taifa la kale la Israeli lilionyesha hivyo.

      Mungu aliwapa Israeli zile Amri Kumi, ambazo za kwanza zilikataza ibada ya mungu mwingine yeyote ila Yehova. Kweli ya msingi ambayo hutegemeza sheria hiyo ni kwamba Yehova aliumba kila kitu. (Kutoka 20:3-5) Lakini je, hilo taifa liliishi kwa kanuni hiyo? Yehova mwenyewe ajibu hivi: “‘Wewe u baba yetu’ [Waisraeli wakaliambia] gogo la mti, [wakalia] ‘Mama’ kwa jiwe. Lakini mimi [Yehova] wamenipa visogo na kugeuza nyuso zao kutoka kwangu.” (Yeremia 2:27, The New English Bible) Ni upumbavu usio na hisia na ukosao kanuni kama nini! Na uliuumiza moyo wa Yehova kama nini!—Zaburi 78:40, 41; Isaya 63:9, 10.

      Wakristo pia wana sheria kutoka kwa Mungu. Kwa kielelezo, wapaswa kuepuka ibada ya sanamu, ukosefu wa adili katika ngono, na utumizi mbaya wa damu. (Matendo 15:28, 29) Ufikiriapo hilo, twaweza kuona kanuni za msingi, kama vile: Mungu hustahili ujitoaji wetu usiohusisha mwingine; twapaswa kuwa waaminifu kwa mwenzi wetu; na Yehova ndiye Mpaji-Uhai wetu. (Mwanzo 2:24; Kutoka 20:5; Zaburi 36:9) Tukifahamu na kuthamini sana kanuni zitegemezazo mielekezo hiyo, twaona kwamba ni yenye manufaa kwetu. (Isaya 48:17) Kwetu sisi, “amri [za Mungu] si zenye kulemea.”—1 Yohana 5:3.

      Ingawa wakati mmoja Waisraeli walipuuza amri za Mungu, kufikia wakati wa Yesu waandishi, “madaktari [wao] wa sheria,” walikuwa wamekuwa wakali mno. Walikuwa wamefanyiza sheria na mapokeo mengi sana yaliyozuia ibada safi na kusitiri kanuni za kimungu. (Mathayo 23:2, NEB) Watu walihisi kwamba wameshindwa, wamekosa tumaini, au unafiki. (Mathayo 15:3-9) Na nyingi za sheria zilizotengenezwa na watu zilikuwa hazina ubinadamu. Alipokuwa karibu kuponya mtu mwenye mkono uliokauka, Yesu aliwauliza Mafarisayo waliokuwapo hivi: “Je, yaruhusika kisheria siku ya sabato kutenda kitendo chema?” Kushindwa kwao kujibu kulifunua kabisa kwamba walihisi lilikuwa jambo lisiloruhusika kisheria, kukifanya Yesu ahisi “akiwa ametiwa kihoro kabisa kwa ukosefu-hisia wa mioyo yao.” (Marko 3:1-6) Mafarisayo wangemsaidia mnyama wa kufugwa (kitega uchumi kifedha) aliyeachwa au aliyejeruhiwa katika siku ya Sabato lakini hawangemsaidia kamwe mwanamume au mwanamke—isipokuwa liwe ni jambo la kufa na kupona. Kwa kweli, walishikilia sana sheria za kibinadamu na mambo madogo-madogo ya kisheria hivi kwamba kama mchwa wanaokimbia haraka juu ya mchoro, walishindwa kuona picha yote—kanuni za kimungu.—Mathayo 23:23, 24.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki