Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Imani Yajaribiwa Huko Poland
    Amkeni!—2000 | Novemba 8
    • Niliendelea na kazi yangu nikiwa mwangalizi asafiriye, na baadaye nilipewa kazi ya kupanga uchapishaji na ugawanyaji wa vichapo vyetu katika Poland.

      Wakati huo, tulitumia mashine za kale za kunakili na mabamba ya nta ya kupigia chapa ili kufanyiza nakala za Mnara wa Mlinzi. Hali ya uchapishaji wetu ilikuwa duni, na tulilazimika kununua karatasi kwa bei kubwa sana kwa sababu ya upungufu wa karatasi wakati huo. Uchapishaji huo ulihitaji kufanywa mahali pa siri, kama vile katika ghala za nafaka, vyumba vya chini ya ardhi, au darini. Wale waliopatikana walihukumiwa kufungwa gerezani.

      Nakumbuka kisima kimoja kikavu tulichotumia. Katika ukuta wake, meta 10.7 chini ya ardhi, kulikuwapo mlango wa kuingilia chumba kidogo ambamo tulifanyiza nakala za magazeti. Ilitubidi kuteremshwa kwa kamba ili kufika humo. Siku moja, nilipokuwa nikiteremshwa kisimani katika ndoo kubwa ya mbao, kamba ilikatika ghafula. Nilianguka hadi chini na nikavunjika mguu. Baada ya kutoka hospitalini, niliendelea kufanyiza nakala za magazeti kwa kutumia mashine hiyo ya kunakili.

  • Imani Yajaribiwa Huko Poland
    Amkeni!—2000 | Novemba 8
    • Nilipoachiliwa huru, nilitumwa Poznan kusimamia “tanuri ya kuoka mikate,” kama tulivyoviita viwanda vyetu vya siri vya uchapishaji. Kufikia mwisho wa miaka ya 1950, uchapishaji wetu ulikuwa umeboreka zaidi. Tulijifunza jinsi ya kupunguza ukubwa wa kurasa kwa kutumia kamera—maendeleo makubwa sana katika uchapishaji wetu—pamoja na kutumia matbaa aina ya Rotaprint. Mnamo mwaka wa 1960 tulianza pia kuchapisha na kujalidi vitabu.

  • Imani Yajaribiwa Huko Poland
    Amkeni!—2000 | Novemba 8
    • Hatimaye, nilipoachiliwa huru, niliwekwa rasmi kuwa msimamizi wa uchapishaji wetu wote katika Poland. Mnamo mwaka wa 1974, baada ya miaka kumi ya kufanya kazi bila kugunduliwa, nilifuatwa na kukamatwa huko Opole.

  • Imani Yajaribiwa Huko Poland
    Amkeni!—2000 | Novemba 8
    • [Picha katika ukurasa wa 20]

      Tulitumia mashine ya kunakili na baadaye tukatumia matbaa aina ya Rotaprint kuchapisha vichapo

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki