Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Matukio Muhimu Ya Mwaka Uliopita
    2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Nchi nyingine ambazo zimepokea matbaa mpya aina ya MAN Roland Lithoman ni Afrika Kusini, Brazili, Japani, Mexico, na Uingereza. Ofisi ya Uingereza ndiyo ya kwanza kuweka matbaa hiyo mpya, ambayo ilifika Julai 2003 na kuanza kufanya kazi Oktoba. Matbaa hiyo huchapa magazeti 750,000 kwa siku, au milioni 1.5, ndugu wakifanya kazi kwa zamu mbili. Idadi hiyo ni mara tatu zaidi ya ile ambayo matbaa ya zamani ilichapa.

  • Matukio Muhimu Ya Mwaka Uliopita
    2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Fundi aliyekuwa akiweka matbaa huko London aliwaambia ndugu hivi: “Nilirudi nyumbani jana jioni na kumwona jirani yangu kwenye bustani yake. Sijawahi kuvutiwa naye, lakini baada ya kuongea naye kwa dakika 20, niligundua kwamba jamaa huyo ni mzuri sana.” Fundi huyo aliongeza kwamba mke wake aliona mabadiliko katika mtazamo na tabia yake, naye akamwambia: “Umekuwa mwenye urafiki, unatabasamu, na kuwasalimu watu.”

      “Nimefanya kazi pamoja na Mashahidi kwa majuma sita,” akajibu. “Na katika majuma mawili yaliyopita sikutumia matusi hata kidogo. Ninatumaini sitayatumia tena.”

      Baada ya matbaa hizo kuwekwa kwenye ofisi ya London, meneja mmoja wa kampuni ya MAN alipigia ofisi hiyo simu na kuwashukuru akina ndugu kwa kuwatunza wafanyakazi wa kampuni hiyo vizuri. Alisema matbaa hizo ziliwekwa bila matatizo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki