Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhukumiwa Mara Mbili Kifungo cha Miaka 25 ya Kazi Ngumu
    Amkeni!—2005 | Desemba 22
    • Wakati huu nilipelekwa katika migodi ya makaa ya mawe ya Vorkuta, iliyokuwa kambi ya kazi ngumu yenye sifa mbaya sana kwenye mwisho wa upande wa kaskazini wa Milima Ural, juu ya Mzingo wa Aktiki.

      Kuepuka Kifo Huko Vorkuta

      Vorkuta lilikuwa gereza kubwa lenye kambi 60 za kazi ya kulazimishwa. Katika kambi yetu tu, kulikuwa na zaidi ya wafungwa 6,000. Watu wengi walikufa kutokana na baridi kali sana, hali mbaya sana za maisha, na kwa sababu ya kuchimba makaa ya mawe chini ya ardhi. Karibu kila siku kulikuwa na watu waliokufa waliohitaji kuzikwa. Afya yangu ilikuwa mbaya sana hivi kwamba singeweza kufanya kazi ngumu ya mikono. Nilipewa kazi iliyosemekana kuwa rahisi zaidi, yaani, kuchota makaa ya mawe na kuyajaza ndani ya tramu zilizokuwa zikingoja.

      Hali zilikuwa mbaya sana huko Vorkuta hivi kwamba wachimba-migodi walipanga mgomo, lakini uligeuka na kuwa uasi. Wachimba-migodi walichagua wasimamizi wao na kupanga kikosi cha wanaume 150 ambao wangekabiliana askari iwapo wangekuja. Walitaka mimi na Mashahidi wengine 30 hivi tujiunge na “jeshi” lao lakini tulikataa.

      Uasi huo uliendelea kwa majuma mawili hadi askari waliokuwa na silaha walipowasili na kuwapiga risasi waasi wote. Tuliambiwa kwamba waasi hao walikuwa wamepanga kutunyonga ndani ya chumba cha kufanya kazi! Inafurahisha kwamba hawakufaulu kutekeleza mipango yao. Unapofikiria mbinu zenye mpango za Wasovieti za kuvunja imani yetu, unaweza kuelewa sababu iliyotufanya tuone kwamba Mungu wetu mkuu, Yehova ndiye aliyetuokoa!

  • Kuhukumiwa Mara Mbili Kifungo cha Miaka 25 ya Kazi Ngumu
    Amkeni!—2005 | Desemba 22
    • [Picha katika ukurasa wa 14, 15]

      Mashahidi wa Yehova katika kambi ya kazi ngumu ya Vorkuta

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki