-
Kukabili Majaribu kwa Nguvu za MunguAmkeni!—2000 | Oktoba 22
-
-
Mnamo Aprili 1958, nilipelekwa kwa kambi nambari 21 ya kazi ngumu, karibu na mji wa Dnepropetrovsk, zaidi ya kilometa 700 kutoka nyumbani ili kumalizia huko muda uliobaki wa kifungo changu. Huko tuliamka saa 12:00 asubuhi, na baada ya kufungua kinywa tulipakiwa kwenye malori, na kupelekwa mahali pa kazi, kilometa 50 kutoka kwa kambi yetu. Tulifanya kazi kwenye ujenzi kwa muda wa saa nane, kisha kurudishwa kambini jioni.
Makao yetu yalikuwa vibanda na kila kimoja kilikuwa na wafungwa 100 hivi. Chakula kilikuwa kibovu na maisha yalikuwa magumu; lakini angalau nilifurahia ushirika wa Mashahidi wawili ambao tuliishi pamoja katika kambi moja. Kila mmoja wetu alijitahidi kutoa kitia-moyo kwa wenzake wawili. Hii ni njia nyingine ambayo Yehova hutumia kuwatia moyo watumishi wake nyakati za taabu—kupitia ushirika wa waamini wenzetu.—2 Wakorintho 7:6.
Kulikuwa na jumla ya Mashahidi 12 kambini. Baadhi yao walikuwa na watu wa ukoo nje ya kambi na hawa walituletea kisiri kurasa za Mnara wa Mlinzi zikiwa zimefichwa ndani ya vifurushi vya chakula. Vingi vya vifurushi hivyo vilikaguliwa na walinzi kabla ya kutufikia. Hivyo, ili kuepuka kurasa hizo za Mnara wa Mlinzi kugunduliwa, zilifungwa kwa karatasi ya plastiki na kuwekwa ndani ya mikebe yenye jemu ambayo hao walinzi hawakujali kuifungua. Mara tu tulipozipokea, tulizinakili kwa mkono na kuzigawanya miongoni mwetu.
Tulijitahidi tuwezavyo kuhubiri juu ya Ufalme wa Mungu, na Yehova alibariki jitihada zetu. Kwa mfano, nilikuja kumjua mfungwa mmoja aliyeitwa Sergei, aliyekuwa mhasibu katika kampuni moja ya serikali katika mashariki ya Ukrainia. Udanganyifu ulipogunduliwa mahali pake pa kazi, alishtakiwa kwa kosa hilo na kufungwa gerezani miaka kumi. Mashahidi kadhaa walijifunza naye hapo gerezani, wakitumia gazeti lolote walilokuwa nalo. Sergei alivutiwa na yale aliyokuwa akijifunza na mwishowe akaniambia hivi: “Nitakapofunguliwa kutoka katika kambi hii, ningependa kubatizwa na kuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova!” Kama alivyokuwa amesema, Sergei alibatizwa punde tu baada ya kutoka gerezani, naye alimtumikia Yehova kwa uaminifu-mshikamanifu hadi kifo chake.
-
-
Kukabili Majaribu kwa Nguvu za MunguAmkeni!—2000 | Oktoba 22
-
-
[Picha katika ukurasa wa 22]
Nikiwa na Mashahidi wenzangu katika kambi nambari 21 ya kazi ngumu
-