-
Yehova Ni Ngome na Nguvu YanguMnara wa Mlinzi—2000 | Februari 1
-
-
Baadaye, kazi ya kuhubiri ikawa kawaida ya maisha yangu na ndivyo na kukamatwa-kamatwa na kufungwa. Si ajabu kwamba yule niliyetazamia kumwoa aliambiwa, “Ukiolewa na yeye, hakika utafungwa gerezani”! Lakini, mambo kama hayo hayakuwa magumu sana. Baada ya kukaa jela siku moja, mara nyingi Shahidi mwingine alitutoa kwa dhamana.
-
-
Yehova Ni Ngome na Nguvu YanguMnara wa Mlinzi—2000 | Februari 1
-
-
Hata hivyo, kadiri nilivyozidi kushiriki katika huduma ndivyo nilivyozidi kutiwa korokoroni. Pindi moja niliwekwa kwenye seli moja na Mike Miller, mtumishi mwaminifu wa Yehova aliyekuwa ametumikia kwa muda mrefu. Tuliketi kwenye sakafu ya sementi na kuzungumza. Mazungumzo yetu yenye kujenga kiroho yaliniimarisha sana. Lakini, baadaye nikawaza, ‘Ingalikuwaje kama hatukuwa tukisikilizana na kuzungumziana?’ Wakati niliotumia pamoja na ndugu huyo mpendwa korokoroni ulinifundisha mojawapo ya masomo mazuri zaidi maishani—twahitaji ndugu zetu na basi twapaswa kuwa wenye kusameheana na wenye fadhili mtu na mwenzake. La sivyo, kama mtume Paulo alivyoandika: “Ikiwa mnafuliza kuumana na kunyafuana, jihadharini kwamba msipate kuangamizana mtu na mwenzake.”—Wagalatia 5:15.
-