Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Urusi
    2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • “Katika nyakati hizo, tulinakili kutoka kwenye nakala halisi, ambazo tulizificha mahali salama. Nakala kadhaa halisi zilifichwa ndani ya jiko, hata kwenye jiko lililokuwa katika ofisi ya msimamizi wa kambi. Ndugu ambao walisafisha ofisi hiyo, walijenga sehemu maalumu katika jiko hilo ambako tuliweka nakala nyingi halisi za Mnara wa Mlinzi. Ingawa wanyapara walitupekua kwa uangalifu sana, sikuzote nakala halisi zilikuwa mahali salama, yaani, katika ofisi ya msimamizi.”

      Akina ndugu walikuja kuwa na ustadi wa kuficha vichapo. Walipenda sana kuficha vichapo kwenye vizingiti vya madirisha. Ndugu hata walificha vichapo kwenye tyubu za dawa ya meno. Ni ndugu wawili au watatu tu waliojua mahali nakala halisi zilipowekwa. Kulipokuwa na uhitaji, mmoja wao alichukua nakala halisi na baada ya kuinakili kwa mkono aliirudisha mahali pake salama. Kwa njia hiyo, sikuzote nakala halisi zilibaki mahali salama.

  • Urusi
    2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • “Wakati mmoja katika Kambi Na. 19 ya Mordvinia, askari wenye mbwa waliwaamuru akina ndugu watoke kambini na wakafanya msako mkali. Kila Shahidi alivuliwa nguo zote, kutia ndani matambara aliyokuwa amevaa miguuni. Lakini akina ndugu walibandika kwa gundi karatasi zilizonakiliwa kwa mkono chini ya nyayo za miguu, na hivyo karatasi hizo hazikugunduliwa. Pia walitengeneza vijitabu vidogo ambavyo vingeweza kutoshea katikati ya vidole. Walinzi walipowaamuru watu wote wainue mikono yao, vijitabu hivyo havikuanguka, na hivyo baadhi ya vichapo hivyo havikupatikana.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki